Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Prof. Ndalichako amuitia Takukuru mkuu wa chuo

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amemtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Diwani Athuman kutuma wataalamu kuchunguza ujenzi wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) pamoja na maafisa wa wizara yake waliosimamia ujenzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Prof. Ndalichako ametoa agizo hilo alipotembelea chuoni hapo kwa ajili ya kukagua ujenzi huo, ambapo alikuta mkandarasi huyo hajakamilisha ujenzi wa majengo hayo tangu apewe kazi hiyo mwaka 2016.

Katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome kumuondoa Mkuu wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM), Paschal Highmagway katika wadhifa wake baada ya kubaini kwamba ametoa taarifa za uongo kuhusu ujenzi huo.

Mkataba wa mkandarasi huyo ulitakiwa kuisha tarehe 5 Aprili 2018 lakini serikali ilimuongezea muda hadi Septemba 15 mwaka huu, lakini alishindwa kukamilisha ujenzi huo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amemtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Diwani Athuman kutuma wataalamu kuchunguza ujenzi wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) pamoja na maafisa wa wizara yake waliosimamia ujenzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Prof. Ndalichako ametoa agizo hilo alipotembelea chuoni hapo kwa ajili ya kukagua ujenzi huo, ambapo alikuta mkandarasi huyo hajakamilisha ujenzi wa majengo hayo tangu apewe kazi hiyo mwaka 2016. Katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome kumuondoa Mkuu wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM),…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram