Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba: Ninaongoza kwa kuwatetea Wazanzibar
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba: Ninaongoza kwa kuwatetea Wazanzibar

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa amesema, ni kinara kwa kuwatetea Wazanzibari. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Prof. Ibrahim amesema, jambo hilo linajieleza vizuri kutokana na historia yake ya kupigania haki na maslahi ya Wazanzibari kuliko kiongozi yeyote wa siasa Tanzania Bara. 

Mwenyekiti huyo amesema hayo leo August 16, 2018 Mjini Unguja kisiwani Zanzibar wakati akizungumza na wanachama wa CUF ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kurejea uenyekiti baada ya kujiuzulu nafasi hiyo tarehe 8 June, 2018.

Amesema kuwa, pamoja na matusi yote aliyotukanwa na wafuasi wa Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho lakini bado historia itaendelea kuonesha kwamba, yeye ndiyo mwanasiasa anayeongoza kuwatetea Wazanzibari kwa upande wa Tanzania Bara.

“Hakuna kiongozi Mwanasiasa wa Tanzania Bara ambaye amekuwa mstari wa mbele kupigania haki za Wazanzibari, maslahi ya Wazanzibari ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzidi Prof. Ibrahim Haruna Lipumba,” amesema.

Katika hatua nyingine Prof. Lipumba amesema, kitendo cha baadhi ya wafuasi wa upande wa Katibu Mkuu Maalim Seif kuhama chama, kinaashiria wazi kwamba hakuna nguvu inayoweza kushindana na CUF Tanzania Bara.

“Hii ni kuonesha Tanzania Bara hakuna aliye upande wa katibu mkuu anayeisumbua CUF,” amesema.

Julius Mtatiro, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF kambi ya Maalim Seif amejiuzulu nafasi hiyo hiyo na kubisha hodi chama tawala-Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!