Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba: Nimeshawishika, nitagombea urais
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba: Nimeshawishika, nitagombea urais

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amesema ameshawishika na atagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe leo tarehe 23 Julai 2020, katika Ofisi Kuu za CUF zilizoko Buguruni, Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu hiyo kutoka kwa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (JUVICUF) Dar es Salaam.

Amesema, alikawia kuchukua fomu ya kugombea urais wa Tanzania ili awape nafasi watu wengine ya kugombea, lakini kwa kuwa vijana hao wamemuomba agombee, atagombea.

“Nilikua nimesita sana kuchukua fomu ili kutoa fusra kwa wanachama wengine wenye nia ya kuchukua fomu kuchukua, sasa vijana wamenishawishi nitagombea sababu sababu na hoja ninazo,” amesema Prof. Lipumba.

          Soma zaidi:-

Kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020, dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu ya kugombea Urais wa Tanzania na Zanzibar, litafungwa tarehe 25 Julai mwaka huu.

Baada ya dirisha hilo kufungwa, Jumatatu ya tarehe 27 Julai 2020, Mkutano Mkuu wa CUF Taifa utafanyika kwa ajili ya kupitisha wagombea wa Urais wa chama hicho Tanzania na Zanzibar.

Ikiwa zimesalia siku mbili kwa zoezi hilo kufika tamati, Prof. Lipumba amekuwa mtu wa pili kukabidhiwa fomu ya kugombea Urais wa Tanzania Bara, akitanguliwa na Chief Lutalosa Yemba. Huku upande wa Zanzibar wakijitokeza watia nia watano.

Waliotia nia kugombea urais wa Zanzibar ni Faki Suleiman Khatib, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar; Abbas Juma Mhunzi, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CUF Zanzibar; Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa; Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mussa Haji Kombo na Rajab Mbarouk.

Akizungumza baada ya kumkabidhi fomu hiyo, Salum Muslim, Katibu wa JUVICUF wilayani Ilala amesema, wameamua kumchukulia fomu mwanasiasa huyo ili kumshawishi agombee.

“Mimi kama kijana ndani ya Dar es Salaam tuliangalia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu zimebaki siku chache takribani siku mbili kumalizika, miongoni mwa watu wamechukua fomu nimejaribu kuwapima tukaona Prof. Lipumba anaweza kuleta changamoto kwenye uchaguzi huu,” amesema Muslim.

Muslim amesema, Prof. Lipumba anafaa kuchuana na Rais John Magufuli, Mgombea Urais wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akidai kwamba, hadi sasa hakuna chama cha upinzani kilichokuwa na mgombea atakayeweza kushindana na mwenyekiti huyo wa CUF.

“Prof. Lipumba anaweza kugombea na mgombea wa CCM, nimeangalia ACT-Wazalendo wametuletea Membe (Bernard Membe), nikimlinganisha Prof. Lipumba hawezi kufanana nao,” amesema Muslim.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!