Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba kummaliza rasmi Maalim Seif
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba kummaliza rasmi Maalim Seif

Spread the love

HARAKATI za Profesa Ibrahim Lipumba kumtosa Maalim Seif, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) zinaelekea ukingoni. Anaandika Faki Sosi … (endelea). 

Kwa sasa Prof. Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini amekamilisha ziara visiwani Unguja na Pemba ambapo taarifa za ndani zinaeleza kuwa, alikuwa akisaka uungwaji mkono kwenye mkutano Mkuu ujao ili kutimiza akidi na kisha kumng’oa Maalim Seif kwenye nafasi ya Ukatibu Mkuu.

Taarifa hizo kutoka pande zote mbili (kambi ya Maalim Seif na ile ya Lipumba) zinaeleza kuwa, dhamira ya Prof. Lipumba ni kuhakikisha Maalim Seif ambaye anaonekana kikwazo, anatimuliwa ndani ya chama hicho ingawa kazi hiyo bado ni ngumu. 

“Kinachofanyika sasa ni kutafuta namna Maalim Seif atavyong’olewa, kule bara Maalim ni mwepesi ila huku Zanzibar ndio shida.

“Huyu (Lipumba) anasaidiwa ndio maana akija msafara wake unalindwa na polisi kama ofisa mkubwa wa serikali. Lengo ni kutengeneza watu ambao watasaidia kukamilisha akidi na hatimaye kumwondoa Maalim Seif,” kimeeleza chanzo chetu rasmi.

Kwa muda mrefu sasa kambi ya Maalim Seif na ile ya Prof. Lipumba imekuwa ikiporomosheana lawama kuhujumiana.

Ni kutokana na kukua kwa mgogoro ndani ya chama hicho ulioanza mwaka 2015 baada ya Prof. Lipumba kujiuzulu uenyekiti na kisha kujerea kwenye nafasi hiyo.

Prof. Lipumba aliwasili Zanzibar Alhamis ya Tarehe 16 Agosti kwa lengo la kufanya mkutano wa ndani na wafuasi wa chama hicho.

Katika harakati zake visiwani humo Prof. Lipumba amefanikiwa kufanya chaguzi za chama kwa ngazi ya kata na wilaya.

Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (Kambi ya Lipumba) amekiri uwepo wa harakati za Prof, Lipumba kufanya mikutano visiwani Zanzibar.

Amesema kuwa, Maalim Seif kwa sasa ametelekeza majukumu yake ambayo kwa muda wote yamekuwa yakifanywa na Magdalena Sakaya ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Bara.

“Tunasimamia Katiba ya chama chetu, Katibu Mkuu akikacha ofisi, nafasi yake itashikiliwa na Naibu Katibu Mkuu ambaye kwa sasa ni Sakaya.

“Kwa kuwa Maalimu Seif ametupa ofisi na majukumu yake basi muda wowote kuanzia sasa tutaita Mkutano Mkuu,” amesema Kambaya.

Kambaya amesema, mkutano huo utachagua viongozi wapya. “Mkutano Mkuu wa chama upo kikatiba na mkutano huu utafanyika mwishoni mwa mwaka huu au mwanzano mwa mwaka na tutafanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya Taifa.”

Hatua hiyo imeelezwa na Salim Biman, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CUF (Kambi ya Maalim Seif) kuwa, Prof. Lipumba anakaidi Katiba ya chama hicho na kwamba, waliochaguliwa hawatotambuliwa na kambi yao.

“Hilo ni genge lake mwenyewe, sisi hatuwatambui, pia hatutatambua chochote kitachofanywa na watu hao kwa kuwa, sio wanachama wa chama wa CUF.” Amesema Biman alipozungumza na mwandishi wa habari hii.

Bimani smeeleza kuwa, Prof. Lipumba hana mamlaka ya kufanya chochote ndani ya CUF na Mahakama imemzuia kuendelea na shughuli za chama.

Bimana amesema, Juni 2019, CUF itafanya Mkutano Mkuu na kumteua mwenyekiti mpya “Mkutano Mkuu wa chama chetu utafanyika Juni Mwaka 2019 na tutafanya uteuzi wa mwenyekiti mpya wa chama.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!