Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Kitila Mkumbo aonyesha rangi yake halisi
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Kitila Mkumbo aonyesha rangi yake halisi

Prof. Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Picha ndogo ni siku ya kuapishwa nafasi hiyo
Spread the love

HATIMAYE Prof. Kitila Mkumbo, aliyekuwa mmoja wa waasisi wa Chama Cha ACT Wazalendo, ameonyesha rangi yake halisi baada ya kutangaza rasmi kujiondoa katika chama hicho cha upinzani, anaandika Shabani Matutu.

Uamuzi huo wa Profesa Mkumbo aliyekuwa akijipambanua kama mpigania harakati za wanyonge na demokrasia nchini unaonyesha wazi sasa ameamua kuwapa wanyonge kisogo na kujikita katika kusimamia kazi zake za u-katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Inaelezwa kwamba wakati kiongozi huyo alipoteuliwa na rais John Magufuli, viongozi wake wa chama walimsihi kukataa uteuzi huo, jambo ambalo hakukubalina nalo na badala yake alitangaza kuachia ngazi ya nafasi ya ushauri aliyokuwa akiishikilia ndani ya chama hicho.

Wakati anaondoka alisema atabaki kuwa mwanachama wa kawaida jambo ambalo lilipingwa na wachambuzi wa kisiasa wakisema ni ngumu kuwa sehemu ya serikali ambayo chama chake cha ACT Wazalendo ni miongoni mwa wapinzani wake.

Prof. Kitila mara kadhaa na chama walikuwa wakipinga hilo kwa kusema kwamba akiwa katika nafasi hiyo atapata nafasi ya kutumikia Ilani ya ACT Wazalendo.

Wakati akiapishwa Ikulu, Dar es Salaam Rais Magufuli alimwambia Kitila kwamba wakati akiwa wizarani anatumikia nafasi yake atafanyakazi zake kwa maelekezo ya Ilani ya CCM.

Jambo hilo lilifanya wachambuzi wengi wa kisiasa kuamini kwamba lazima Profesa Mkumbo angefika wakati wangeanza kusuguana na chama chake cha ACT -Wazalendo, katika misimamo.

Hilo limetokea hivi karibuni baada ya mwanasiasa huyo kutabiri kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2020, atapita bila kupingwa kutokana na kazi aliyoifanya ya kusambaza maji maeneo mbalimbali.

Kauli hiyo ilipingwa na Chama cha ACT -Wazalendo kupitia kwa Katibu wake mwenezi, Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi aliyesema rais Magufuli atakuwa na hali ngumu katika uchaguzi ujao kutokana na kufanya nchi kuwa na hali ngumu.

Baada ya matukio hayo hatimaye Profesa Mkumbo ameamua kuandika barua ya kutangaza kujiondoa katika uanachama kwa kile alichosema kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi anaoupata kwa kutumikia Ukatibu Mkuu wa wizara.

“Katika maelezo niliyoyaandika hapo juu na ili kuepuka mgongano wa wazi wa maslahi, nimeamua kung’atuka uanachama wangu wa ACT- Wazalendo,”, ilisomeka sehemu ya barua hiyo.

Amesema uamuzi zaidi anauachia uongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, na huku akiwashukuru kwa ushirikiano kwa muda wote ambao walikuwa kwenye chama.

Mwanasiasa huyo alikuwa miongoni mwa wanachama watatu waliofukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia kikao cha dharura kilicofanyika Dar es Salaam kati ya tarehe 3-4 Januari, 2014.

Watuhumiwa wote watatu walishtakiwa kwa jumla ya mashtaka 11 yanayohusu ukiukwaji wa vifungu mbali mbali vya katiba ya chama, kanuni za uendeshaji wa kazi za chama, kanuni za kusimamia shughuli, na mwenendo na maadili ya wabunge.

Mashtaka yote yalitokana na watuhumiwa kuandaa kile kilichokuwa kikiitwa mkakati wa mabadiliko ambayo yalikuwa na lengo la kukashifu viongozi wakuu wa chama, yaani mwenyekiti wa taifa, Freeman Mbowe na aliyekuwa Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!