Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Assad: Inapaswa kusimamia misingi ya kazi
Habari za Siasa

Prof. Assad: Inapaswa kusimamia misingi ya kazi

Spread the love

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad amesema, maofisa wanatakiwa kufanya kazi kwa kujiamini pia kujibu hoja kwa wakati. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mabaraza ya CAG, jijini Dodoma leo tarehe 14 Mei 2019 Prof. Assad amesema, ni wajibu kwa kila mtumishi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa wakati na kusimamia misingi ya kazi zao.

Pamoja na kutaka watumisi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa kujiamini pia amesema wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosekana rasilimali fedha na rasilimali watu.

Akizungumzia rasilimali fedha amesema kuwa, imesababisha kukosekana kwa vyombo vya usafiri vya kutosha hivyo kusababisha kazi kwa ugumu.

Prof. Assad amesema, usafiri unahitajika katika maeneo ya ukaguzi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Profesa Asad ametoa kauli hiyo wakati wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo, lililofanyika jijini Dodoma.

Amesema, hakuna sababu ya kuwa na woga katika utendaji wao, bali wanapaswa kuwa mfano ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Mbali na hilo amewapongeza viongozi waliochaguliwa kwa ajili ya kuongoza baraza hilo na kuwataka kutenda kazi na sio kubweteka.

Amesema, wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanasukuma gurudumu hilo kwa maslahi ya wafanyakazi.

“Nawaomba mchape kazi na si kubweteka,” amesema Professa Asad.

Mgeni rasmi katika baraza hilo Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Francis Michael amesema, utovu wa nidhamu, rushwa katika mabaraza havitakiwi.

Amesema, kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii ili waweze kusaidia wafanyakazi kwa ujumla.

Naibu hiyo amesema, bajeti inatakiwa ijadiliwe na baraza kabla ya kupelekea bungeni ili kuhakikisha wanaitendea haki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!