Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wauwa watu wanne
Habari Mchanganyiko

Polisi wauwa watu wanne

SACP Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam
Spread the love

JESHI la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeuwa watu wanne kwa risasi wakidai kuwa ni majibizano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo terehe 18 Agosti 2020 na Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda hiyo, SACP Lazaro Mambosasa kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

Mambosasa amesema, jeshi hilo limeuwa watu hao kwenye majibizano ya risasi saa 9:30 tarehe 15 Agosti 2020 .

“…tulifanikiwa kukamata silaha moja bastola aina ya Bereta iliyofutwa namba zake za usajili ikiwa na risasi moja ndani ya magazine na maganda manne ya risasi, tochi moja na milipuko miwili iliyotengenezwa kienyeji,” amesema Mambosasa.

Amesema, awali jeshi hilo lilimshikilia Nuru Thadei (34), aliyetajwa kuhusika na matukio ya uhalifu ikiwa pamoja na tukio la mauaji ya mchina mwaka 2011 eneo la Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Mambosasa amesema, Thadei alivyohojiwa, alikiri kuhusika na matukio hayo na kuwaongoza askari wa jeshi hilo mpaka kwenye nyumba ya maficho ya wenzike watatu.

Baada askari kufika eneo hilo, Thadei alipiga kelele ya kutoa ishara kwa wenzake na ndio walipoanza kurusha risasi kuelekea walipo askari, walijibu na kusababisha kujeruhi watu hao ambapo kabla ya kufikishwa hospitali, walishafariki dunia.

Mbali na Thadei, wengine ni pamoja na Godfrey Faustine, Antony Mnyamongo na Peter Mseba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!