Ndege ya Bombardier aina ya Q400

Polisi watinga nyumbani kwa Lissu kusaka barua ya Bombardier

MAOFISA wa jeshi la polisi wamekwenda nyumbani kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpekua, anaandika Hellen Sisya.

Jana Lissu alikamatwa na polisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu na kupelekwa kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam.

Lissu anatuhumiwa kwa makosa mawili ambayo ni kumkashfu Rais John Magufuli ( kusema makosa ya Rais hadharani) na la pili ni uchochezi kwa kutoa taarifa kuhusu ndege inayoshikiliwa nje ya nchi.

Update

Makachero wa polisi wazingira kwa Lissu

Maaskari wa jeshi la polisi bado wametanda nyumbani kwa mbunge wa Singida mjini, Tundu Lissu, eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam, wakiendelea na upekuzi ambao hata hivyo haujajulikana ni wa nini.

Kuna tetesi kwamba huenda makachero hao wanasaka nyaraka muhimu ama barua zinazohusu taarifa alizotoa Lissu kuhusu ndege ya Bombardier. kushikiliwa nje ya nchi.

Jana Lissu alikamatwa na kushikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam na leo asubuhi kulikuwa na tetesi kwamba angepelekwa mahakamani , lakini baadaye ikajulikana hakupelekwa huko.

MAOFISA wa jeshi la polisi wamekwenda nyumbani kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpekua, anaandika Hellen Sisya. Jana Lissu alikamatwa na polisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu na kupelekwa kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam. Lissu anatuhumiwa kwa makosa mawili ambayo ni kumkashfu Rais John Magufuli ( kusema makosa ya Rais hadharani) na la pili ni uchochezi kwa kutoa taarifa kuhusu ndege inayoshikiliwa nje ya nchi. Update Makachero wa polisi wazingira kwa Lissu Maaskari wa jeshi la polisi bado wametanda nyumbani kwa mbunge wa Singida mjini,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Masalu Erasto

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube