JESHI la polisi limewakamata watu kadhaa ambao walikuwa wakipita katika ofisi za makao makuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) zilizopo eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es salaam huku wakiwa wamevalia t shirt zilizoandikwa “Pray For Lissu”, anaandika Hellen Sisya.
Polisi hao ambao walikuja na magari yasiyopungua sita huku wakiwa na silaha, walizingira ofisi hizo kwa takribani masaa matatu kuanzia saa tisa mchana mpaka saa kumi na moja jioni hii huku wakihoji kila mtu ambaye alikuwa akifika katika ofisi hizo.
https://youtu.be/sZ9CI1nJs4Q
Mapema Leo hii jeshi la polisi lilizingira viwanja vya Tip vilivyopo eneo la Sinza, mahali ambapo chama hicho kilitarajiwa kufanya maombi kwa ajili ya mwanasheria mkuu Wa chama hicho Tundu Lissu ambaye anaendelea na matibabu nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi wiki iliyopita mjini Dodoma.
Leave a comment