Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wamtaka Rungwe kuripoti Oysterbay
Habari za Siasa

Polisi wamtaka Rungwe kuripoti Oysterbay

Spread the love

JESHI la Polisi limemtaka Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa Chama cha Umma (CHAUMMA) kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay leo tarehe 3 Juni 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).  

Rungwe ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa vyama vinane vya upinzani, alipokea wito huo jana tarehe 2 Juni 2019.

Ni muda mfupi baada ya Rungwe kuzungumza na wanahabari kuhusu msimamo wa vyama hivyo kutoshiriki uchaguzi mdogo wa madiwani, uliopangwa kufanyika tarehe 15 Juni 2019 katika kata 32.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Rungwe anaitwa polisi kutokana na mkutano wake na waandishi alioufanya jana kwenye Makao Makuu ya chama chake Makumbusho, jijini Dar es Salaam.

Kwenye mkutano wake, Rungwe alisema kuwa, vyama hivyo vinane ambavyo ni Chadema, Chauma, NCCR-Mageuzi, UPDP, CCK, DP, ACT-Wazalendo na NLD havitashiriki uchaguzi huo mpaka pale Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), itakapotekeleza hukumu ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam ya kutoruhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi.

Alisema kuwa, wakurugenzi hao wamekuwa wakiwaandikia barua kuwaeleza utaratibu wa kuchukua fomu na kurejesha, huku wakitia saini kama wasimamizi wakuu kinyume na matakwa ya kisheria kwa mujibu wa hukumu hiyo.

“Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa kwenye magari matatu walifika ofisi ya CHAUMMA baada ya Press Conference ya viongozi wakuu wa vyama vinane vya upinzani, walimpa taarifa kwamba anatakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oyesterbay, tarehe 03 Juni 2019.

“Polisi hao wanadai kuwa, Mheshimiwa Rungwe anahitajika na Mkuu wa Polisi Kinondoni (RPC-Kinondoni), kutokana na mkutano wake na wanahabari.

“Viongozi waandamizi wa vyama hivyo, waliweka msimamo wa pamoja wa kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio kwenye kata 32 unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 Juni 2019 kwasababu, unasimamiwa na wakurugenzi kinyume na uamuzi wa Mahakama Kuu,” ilieleza taarifa ya Tumaini Makene, msemaji wa Cahdema.

Rungwe mwenyewe amethibitisha kupokea wito wa polisi na kwamba, ataitikia kama sheria inavyoelekeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!