Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Tabora kuwasaka watu wanaotaka kujinyonga
Habari Mchanganyiko

Polisi Tabora kuwasaka watu wanaotaka kujinyonga

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Tabora limesema litafanya doria ya kuwabaini watu wanaotaka kujinyonga, kisha kuwafikisha mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Barnabas Mwakalukwa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, wakati akizungumza na wanahabari, amesema hatua hiyo itasaidia kukomesha matukio ya watu kujinyonga.

“Basi niwaambie mwaka huu tabia hizo zikome, kwa wale wanaotegemea kujinyonga, sisi tutawakamata kabla ya kujinyonga  halafu tutawapeleka mahakamani. Tutaanza kufanya doria kuhakikisha kwamba wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu tuwakamate,” amesema Kamanda Mwakalukwa.

Wakati huo huo, Kamanda Mwakalukwa amewaomba viongozi wa dini, kutoa ushauri nasaha kwa waumini wao, hasa wenye matatizo ya kiafya na migogoro mbalimbali, ili kudhibiti matukio ya watu kujinyonga.

“Na pia tuna waomba viongozi wa taasisi za kidini wafanye doria za kiroho, ili waweze kuzima matukio ya namna hiyo kwa kutoa nasaha na elimu. Pia wale wataalamu wa ushauri nasaha waende kwa watu wenye matatizo ya kiafya, kuchanganyikiwa kwa akili, ili wawape faraja,” amesema Kamanda Mwakalukwa na kuongeza;

“Kwamba pamoja na matatizo waliyonayo ya kiafya ,  kiuchumi ,  kisiasa,  migogoro ya kijamii na ya kifamilia, bado wana kuwa na nafasi nzuri ya kuwa na maisha bora baada ya kupewa ushauri nasaha, mara nyingine tunapoteza watu muhimu katika ujenzi wa nchi yetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!