Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi, ACT-Wazalendo wavimbiana
Habari za Siasa

Polisi, ACT-Wazalendo wavimbiana

Spread the love

JESHI la Polisi nchini, limekataza kufanyika maandamano ya tarehe 9 Aprili 2019 yaliyopangwa na Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wakati jeshi hilo likikataza maandamano hayo, ACT-Wazalendo wameeleza kuwa, watafanya kwa kuwa ni haki yao ya kikatiba.

Tarehe 6 Aprili 2019 Isack Nyasilu, Katibu wa Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo, alitangazakufanya maandamano kesho tarehe 9 Aprili, 2019 kupinga azimio la bunge la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Taarifa hiyo ya zuio la polisi imewekwa leo tarehe 8 Aprili 2019 katika ukurasa wake wa Twitter wa ACT-Wazalendo ikieleza kuwa, polisi wamepiga marufuku maandamano hao.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amezuia maandamano hayo.

Licha ya zuio hilo, Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo imesema, utaratibu wake katika kushiriki maandamano hayo uko pale pale.

“Tumepokea taarifa RPC wa Dodoma kuwa amezuia maandamano ya Ngome, Jumuiya na Mabaraza ya Vijana ya Vyama vya siasa.

“Tunapenda kumjulisha kuwa, sisi kama Social Auditors tunahaki ya kuhoji na kusimama na CAG, tunaendelea na maandamano kama yalivyopangwa kwa kuwa, ni haki yetu ya kikatiba,” inaeleza taarifa ya Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, utaratibu wa usafiri wa kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Singida na Iringa kwenda Dodoma kushiriki maandamano ya tarehe 9/4/19 upo kama ulivyopangwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!