Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole: Vitambulisho vya machinga havitafutwa
Habari za Siasa

Polepole: Vitambulisho vya machinga havitafutwa

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

HUMPHREY Polepole, Katibu wa Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), nchini Tanzania amesema, Serikali ya chama hicho haitaviondoa vitambulisho vya mjasiriamali ‘machinga’ kwa kuwa vinatija kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Polepole amesema hayo leo Ijumaa tarehe 25 Septemba 2020, jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yaliyojitokeza kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.

Amesema vitambulisho hivyo vimewaokoa wananchi kwenye adha ya kulipa Sh.180,000 kwa mwaka na badala yake wanalipa Sh. 20,000

“Mama anayeuza ndizi pale Nyamagama, mama anayeuza uji pale Kariakoo kijana anayeuza madafu mtaa wa Lumumba pale Dar es Salaam akipita mgambo wa Halmashuri wanalipa Sh.500 mpaka Sh.1,000 kwa siku kwa mwaka inakuwa Sh.180,000 Rais John Magufuli akasema walipe Sh.20,000 kwa mwaka mzima,” amesema Polepole.

Polepole amesema vitambulisho hivyo vimewapa tija na huru kwenye biashara zao na kuwabeza wagombea wengine wanaojinadi kwa wananchi kwamba wakichaguliwa watavifuta jambo ambalo amesema, litawasababishia gharama wafanyabiashara hao.

“Angalia wajasiriamali walivyopendeza ndio uelewe Rais Magufuli kwanini watu wanyonge wanampenda, kwa sababu anajua lugha yao, anajua changamoto zao anajua shida zao,” amesema.

“Kuna mtu anasema tukija tutafuta vitambulisha kwa hiyo utafuta vitambulisho turudi kwenye kulipa Sh.180,000, tulianza kuhangaika kurasimisha biashara za wanyonge kitu tulichofanikiwa ni pamoja na kutoa utambulisho mahsusi kwa mjasiariamali,” ammesema

Amesema kitambulisho cha mjasiriamali kimerasimishwa kisheria na kuwafanya kina mama, vijana na watu wenye ulemavu kupata mkopo usiokuwa na riba kwenye Halmashauri.

Wakati huo huo, Polepole amesema madai ya wapinzani kuwa wahudhuriaji wanaojaza mikutano ya CCM wanapelekwa kwenye viwanja vya kampeni kwa kubebwa kwa kwenye mabasi yaliyokodiwa hayana ukweli wowote.

“Mfamaji haishi kutapata, mikutano ya CCM inawatu wengi mno, wanahabari ni mashuhuda, wanasema watu hawa wameletwa, mnakumbuka siku ilivyojaa CCM Kirumba basi ngapi zitaweza kujaza uwanja ule, wanadanganya vitu vya waziwazi,” amesema Polepole.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!