Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole amchimba mkwara Maalim Seif
Habari za Siasa

Polepole amchimba mkwara Maalim Seif

Humphrey Polepole, akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

HUMPHREY Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amemtaka Maalim Seif Sharif Hamad kuacha kuchafua viongozi wa chama hicho, vinginevyo atashughulika naye. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Bila ya kumtaja jina, Polepole amesema ‘Mzee Yule’ amekuwa na tabia ya kuchafua viongozi wa chama hicho.

Polepole ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020, wakati akitaja orodha ya wagombea uwakilishi visiwani humo.

“Anatupotezea muda saa hizi, anasema mgombea wetu, acha. Mimi huwa sina taratibu ya kusema wazee, acha hii ni mara ya mwisho.”

“Nitashughulika na wewe katika namna ambayo italeta habari nyingine, acha kabisa tufanye siasa za kistaarabu na sisi tumefungua kampeni, hatutaki kusema watu tunasema hoja,” amesema Polepole.

“Lakini tunajua tunao mahasimu wetu, watu ambao kwa kweli hawatutakii mema na leo sikutaka kumsema yeyote na sitafanya hivyo na hasa katika nyumba ya CCM ni heshima kubwa lakini tunatoa rai moja tu, Mzee yule aache kutaja majina ya viongozi wetu ,” amesema Polepole.

Polepole amesema, onyo hilo ni la mwisho kwake na kwamba afanye siasa za kistaarabu.

“Unajua sisi CCM kazi kuwa tumeipiga na tunatambua itakuwa ngumu sana kwa vyama vingine kufanya siasa ya kueleweka kwenye uchaguzi huu, sababu hoja ya kuuza haipo basi wajipange na si kutengeneza hoja ya kubumbabumba,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!