Paul Pogba

Pogba aambukizwa corona, atoswa Ufaransa

Spread the love

PAUL Pogba, kiungo wa Manchester United, ameachwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Ufaransa, baada ya kubainika kuambukizwa virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea)

Kikosi hicho cha Ufaransa kitacheza michezo miwili ya kirafiki na Sweden tarehe 5 Septemba 2020 na mchezo wa pili kitacheza nyumbani Paris 8 Septemba 2020.

Mchezaji mwingine ambaye ameachwa katika kikosi hicho baada ya kukutwa na  corona ni kiungo wa Tanguy Ndombele wa timu ya Tottenham Hotspur ya Uingereza.

Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps amesema, ameamua kufanya mabadiliko ya kumwita kikosini Eduardo Camavinga wa timu ya Rennes ya Ufaransa kuchukua nafasi ya Pogba ambaye jana alipimwa na kukutwa na corona.

Paul Pogba

Wawili hao wamelazimika kusalia Uingereza kwa mujibu wa taratibu, wanapaswa kujitenga kwa siku 14.

Hatua hiyo, inawafanya wachezaji hao kila mmoja kukosa maandalizi ya msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) itakayoanza tarehe 12 Septemba 2020.

PAUL Pogba, kiungo wa Manchester United, ameachwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Ufaransa, baada ya kubainika kuambukizwa virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea) Kikosi hicho cha Ufaransa kitacheza michezo miwili ya kirafiki na Sweden tarehe 5 Septemba 2020 na mchezo wa pili kitacheza nyumbani Paris 8 Septemba 2020. Mchezaji mwingine ambaye ameachwa katika kikosi hicho baada ya kukutwa na  corona ni kiungo wa Tanguy Ndombele wa timu ya Tottenham Hotspur ya Uingereza. Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps amesema, ameamua kufanya mabadiliko ya kumwita kikosini Eduardo Camavinga wa timu ya Rennes ya Ufaransa kuchukua…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!