Thursday , 25 April 2024
Habari za Siasa

Pigo lingine Chadema

Edward Sembeye, Mkuu wa Mawasiliano ya Umma NCCR-Mageuzi
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinaendelea kukimbiwa na baadhi ya makada wake muhimu, tena waliokuwa na mamlaka. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Edward Sembeye, aliyekuwa Katibu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), leo tarehe 26 Februari 2020, ametangaza kujitenga na chama hicho na kwamba anapumzika siasa.

Mbele ya waandishi wa habari, Sembeye amesema moja ya vitu vinavyokiumiza chama hicho, ni chama hicho kwenda ama kuendeshwa kwa mdundo wa Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho na si Katiba ya Chadema.

“Leo mambo ya Chadema yanaamuliwa kwa mujibu wa kauli na amri za Mbowe (Freeman Mbowe), sio Katiba. Mwenyekiti ameamua kugeuzi chama kuwa mali yake binafsi.

“Lakini tukitoka nje tunawaaminisha umma wa Watanzania kwamba chama hiki ni mali ya Watanzania. Kuna mambo mengine kiuongozi, tunapaswa kuwa na akiba ya maneno,” amesema.

Amesema, kutokana na kutokuwa na umoja na msimamo, matokeo yake wamepoteza hata majiji waliyokuwa wakiyaongoza.

“…tumechukua Jiji la Dar es Salaam, tumechukua Jiji la Arusha, leo tumeyapoteza majiji yote na bado tunawaambia Watanzania kuwa bado tupo imara,…” amesema.  

Sembeya ameonesha kukerwa na maneno ya kejeli yanayotolewa na viongozi wa Chadema pia wajumbe wa Kamati Kuu, akisema jambo hilo si la kistaarabu.

“Juzi nimeona mjumbe mmoja wa Kamati Kuu akisema yule aliyehama ni panya,…

“Dhumuni la chama chetu ni kutetea haki za binadamu, kumwita mtu panya kwa sababu ameondoka kwenye chama chako! Kuna watu wameitwa wanaume suruali, mtu huyu ni Mjumbe wa Kamati Kuu,” amesema.  

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!