Tuesday , 19 March 2024
Home Kitengo Michezo Peter Tino, Mutebezi waipa somo Stars
Michezo

Peter Tino, Mutebezi waipa somo Stars

Spread the love

WACHEZAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Peter Tino na Taso Mutebezi, wamewataka wachezaji wa sasa wa timu ya Taifa kuivunja rekodi yao walioiweka miaka 39, kwa kuifunga Uganda siku ya jumapili kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la mataifa (AFCON). Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Kwa upande wa Mutebezi alisema kuwa, ni muda sasa wa kuwahamisisha vijana kusudi waweze kuvunja hiyo rekodi yao walioiweka mwaka 1980 wakati walipoifanikisha Taifa Stars kucheza michuano ya AFCON kwa mara nchini Nigeria.

“Tumekuja kuwa hamasisha vijana kusudi waweze kuvunja rekodi yetu tangu wakati ule miaka 39 imepita Tanzania haijawahi kufanya hivi kwa hiyo tumekuja kuwapa hamasa vijana waweze kufanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya Uganda” alisema Mutebezi ambaye alikuwa moja ya wachezaji waliocheza michuano hiyo 1980.

Mutebezi aliongezea kuwa haoni sababu ya kushindwa kuapata matokeo katika mchezo huo kutokana na wachzaji wa sasa wanapewa kila kitu ikiwemo posho , kambi nzuri na motisha tofauti na wao wakati walipokuwa wakicheza.

Nae Peter Tino ambaye alikuwa mmoja ya wachezaji wa zamani waliokuja kuangalia mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam alisema kuwa haiwezekani toka miaka hiyo iwe historia  kwa timu yetu kushiriki michuano hiyo, sasa ni muda kwa wachezaji wa sasa kuandika historia mpya.

“Haiwezekani toka mwaka 1979/1980 mpaka leo iwe tu Peter Tino katupeleka Lagos, tuanataka sasa ibadilike ndio maana tumekuja hapa kuawapa motisha na moyo vijana wetu kwa sababu uwezo wanao na nafasi wanayo” alisema Peter Tino.

Ikumbukwe Peter Tino ndiye aliyeifungia bao Tanzania bao la pekee lililo wapelekea Lagos, Nigeria kwenye michuano ya AFCON kwenye mchezo uliochezwa mjini Lusaka dhidi ya wenyeji Zambia.

Kwa sasa Stars ina pointi tano na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L, mara baada ya kucheza michezo mitano ikiwa sawa na Lesotho nao wenye pointi kama hizo wakitofautiana mabao ya kufungwa na kushinda.

Ni miaka 39 imepita tangu mara ya mwisho timu ya Taifa ya Tanzani kufuzu katika michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika, wakati huo kikosi cha Stars kilikuwa na nyota kama Athumani Mambosasa, Juma Pondamali, Taso Mutebezi, Jelah Mtagwa, Leodgar Tenga.

 

Mohamed Kajole, Husein Ngulungu, Mtemi Ramadhan, Juma Mkambi, Omari Hussein, Mohamed Masewa, Thuweni Ally, Peter Tino, Ahmed Thabit, Charles Boniface, Salim Amiri, Adolf Richard, Zamoyoni Mogela, Martin Kikwa na George Kulagwa.

Tazama video kamili hapo chini

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Tusua kijanja na mechi za Europa leo

Spread the love  Alhamisi ya leo EUROPA inaendelea ambapo ni mechi za...

Michezo

Hapa Diego Simeone, pale Simeone Inzaghi kivumbi cha Ligi ya Mabingwa Ulaya

Spread the love LIGI ya Mabingwa ulaya itaendelea usiku wa leo ambapoitakwenda...

error: Content is protected !!