Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Passport ya Bulaya yaahirisha kesi
Habari za SiasaTangulizi

Passport ya Bulaya yaahirisha kesi

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, imeahirisha kusikiliza kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa Chadema, kutokana na upande wa mashtaka kumtaka mshtakiwa wa tisa, Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, kuwasilisha mahakamani hapo hati ya kusafiria ili kuendelea kumhoji juu ya ushahidi wake. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Katika kesi hiyo namba 112 la mwaka 2018, Bulaya anashtakiwa pamoja na viongozi wanane wa chama hicho akiwemo, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa, Vicent Mashinji, Katibu Mkuu Chadema-Taifa, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Bara na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Zanzibar.

Wengine ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini, Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini.

Leo tarehe 6 Desemba 2019, Bulaya akiohojiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon ameeleza kuwa tarehe 17 Februari, 2019, alimsindikiza Mdee kwenye hospitali ya St. Parrot nchini Afrika Kusini, kwa ajili ya matibabu.

Bulaya ameulizwa aina gani ya hati ya kusafiria aliyoitumia wakati alipomsindikiza hospitali Mdee amejibu kuwa ni hati ya kawaida.

Wankyo amemuuliza Bulaya iwapo upande wa mashtaka ukiitaka kuiona hati yake kusafiria amejibu kuwa siku yoyote kesi hiyo ikitaja ataiwasilisha.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameiomba mahakama hiyo kuhairisha shauri hilo ili Bulaya akiwasilisha hati ya kusafiria ndipo wataendelea kumhoji.

Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 19 na 20 Desemba mwaka huu.

Washtakiwa wote wanatuhumiwa kwa makosa ya kutoa maneno ya uchochezi, kufanya kusanyiko lisilohalali na kufanya maandamano kinyume cha sheria yaliyodaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwelina Akwelin.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

Regina Mkonde: CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!