Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Tumaini Maligana

Pari Match waikogesha Mamilioni Mbeya

Spread the love

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Pari Match imeingia mkataba na klabu ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh. 270 milioni kama mdhamini mkuu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkataba huo ambao utaanza leo 28 Agosti, 2020 utakuwa wa mwaka mmoja katika msimu wa Ligi wa 2020/21.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Tumaini Maligana amesema kuwa wameingia mkataba na klabu hiyo kwa kuwa ni mmoja ya klabu ambayo inaushawishi mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini kutokana na ukubwa wake.

“Tunapenda kuitambua kwamba Mbeya City ni mmoja ya klabu kubwa Tanzania hususani ukiangalia idadi ya mashabiki lakini pia ushawishi katika soka.”

 

“Mkataba huu unathamani ya Sh. 270 milioni, lakini thamani nzima ya mkataba inazidi kutokana na sababu mmoja, tutakuwa na program ya promosheni na klabu hiyo ambayo itakuwa na thamani si chini ya Sh. 200 milioni,” alisema Tumaini.

Kwenye tukio hilo, Mbeya City iliwakilisha na Mtendaji Mkuu wao, Emmanuel Kimbe amesema kuwa amewashukuru kampuni hiyo kwa kuwaunga mkono kwa kuwa uendeshaji wa klabu nyingi unagharama kubwa hivyo kupata wadhamini wanawezesha uwendeshaji wa shughuli za kila siku kuwa rahisi.

“Uendeshaji wa klabu unachangamoto nyingi hasa gharama, unapopata wadau wanarahisisha wa klabu na ushiriki wa mashindano mbalimbali kwa kuwa unaongeza thamani ya mpira wetu, na sisi tunawaahidi kwa msimu huu tutafanya kazi vizuri na kuwapa ushirikiano mkubwa,” alisema Kimbe.

Ikumbukwe Mbeya City ilipanda Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye msimu wa 2013/14 na kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Pari Match imeingia mkataba na klabu ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh. 270 milioni kama mdhamini mkuu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). Mkataba huo ambao utaanza leo 28 Agosti, 2020 utakuwa wa mwaka mmoja katika msimu wa Ligi wa 2020/21. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Tumaini Maligana amesema kuwa wameingia mkataba na klabu hiyo kwa kuwa ni mmoja ya klabu ambayo inaushawishi mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini kutokana na ukubwa wake. “Tunapenda kuitambua kwamba Mbeya City ni mmoja ya klabu kubwa Tanzania hususani…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!