Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Pamoja na madhira niliyopitia bado niko imara – Kubenea
Habari za Siasa

Pamoja na madhira niliyopitia bado niko imara – Kubenea

Spread the love

MBUNGE mahiri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), katika jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amedaikuwa pamoja na vitimbwi na mateso anayopitia, badoataendelea kusimama imara kulinda hadhi na heshimawaliyompa wananchi wa jimbo lake. Anaripoti MwandishiWetu…(andelea).

Akizungumza katika mkutano na viongozi wa Chademakutoka katika nane za jimbo la Ubungo, Kubenea alisema, tangu alipochaguliwa kuwa mbunge wa Ubungo, 25 Oktoba2015, amepitia misukosuko mingi.

Ametaja baadhi ya misukosuko hiyo, kuwa ni pamoja nakushitakiwa mahakamani na kutiwa hatiani, kufungiwamagazeti yake na kuzuiwa kushiriki mikutano ya Bunge.

Hata hivyo, mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwandishi wahabari na ambaye tarehe 5 Januari 2008, alivamiwa nakumwagiwa tindikali machoni amesema, “lakini yote hayo, kamwe hayawezi kunirudisha nyuma.

Alisema, “tangu nilipochaguliwa kuwa mbunge wa Ubungo, nimepitia madhira makubwa sana. Nimekumbana navitimbiwi vingi, ikiwamo kuzuiwa kuhudhuria mkutano waBunge kwa muda na kufutwa kwa mikutano ya hadharadakika za mwisho.

“Kuna wakati nilikamatwa na polisi, nikawekwa lupango, nikashitakiwa mahakamani na kisha nilitiwa hatiani, baada yakukwaruzana na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ambaye sasa ni mkuu wa mkoa wa Dar esSalaam. Yote hayo, ni kwa sababu, mimi ni mbunge waupinzani.”

Ameongeza, “…lakini nawahakikishia kuwa pamoja navikwazo na vigingi vyote hivyo, bado niko imara nanitaendelea kuwatumikia na kulinda heshima mliyonipa yakunichagua mbunge wenu kupitia Chadema.”

Mkutano kati ya Kubenea na viongozi hao, ulifanyikaJumapili iliyopita, katika ukumbi wa mikutano wa Moshi Hoteli, Manzese, jijini Dar es Salaam. Ulihudhuriwa naviongozi mbalimbali wa kata, wenyeviti wa serikali za mitaana wajumbe wao, madiwani na baadhi ya watia nia wauchaguzi ujao wa mitaa.

Akizungumzia uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, aliwaombawajumbe waliohudhuria kushiriki kikamilifu katika uchaguzihuo. Alisema, anatambua ugumu uliyopo katika uendeshajiwa uchaguzi hizo, ikiwamo uwapo wa sheria kandamizi, lakini akaahidi kusimama pamoja nao katika kuhakikishaushindi unapatikana.

Akiongea kwa hisia kali, Kubenea alisema, “…natambuamatatizo yaliyopo na tambua changamoto zilizopo. Lakininawahakikishia, kwamba pamoja na matatizo hayo, nitahakikisha tunashinda uchaguzi huo.”

Akizungumzia madhira mbalimbali aliyopita, mbunge huyoamekumbushia tukio lake la kukamatwa na kushitakiwawakati akiwa anatekeleza majukumu yake. Alilitaja tukiomoja wapo, kuwa ni lile la kukamatwa kwake, wakatialipokwenda kutembelea eneo la biashara huru – Export Processing Zone (EPZ) – lililopo eneo la Makuburi.

Nikiwa katika eneo hilo, ndipo tulipotifuana na aliyekuwamkuu wa wilaya ya Kinondoni, ndugu Paul Makonda ambayewakati huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Makondaalitaka kuninyanyasa na kutumia madaraka yake vibaya. Nilimkatalia,” ameeleza Kubenea.

Amesema, “sikushangaa. Hii ni kutokana na hulka yake yakutotambua na kutoheshimu viongozi wenzake, hasa wale waliochaguliwa moja kwa moja na wananchi.

Nikiwa mbunge ninayejitambua, nilisimama kidete kupingaudhalilishaji huo. Hatua yangu hiyo, ilinisababishakukamatwa na kushitakiwa mahakamani. Nayo mahakamailinitia hatiani na kunihukumu adhabu ya kutofanya kosa kwamuda wa miezi mitatu.”

Kubenea alitumia fursa hiyo, kuwashukuru viongozi hao kwamchango wao mkubwa katika ujenzi wa chama hicho naushirikiriano wanaompatia katika kutimiza majukumu yake.

Alisema, mkutano wake huo, mbali na kulenga kukutana naviongozi hao, ulikuwa mahususi kutoa taarifa ya kazi zakekatika kipindi cha miaka minne ya ubunge wake.

Alisema, “nafahamu kuwa baadhi ya viongozi wenzetu ndaniya Chadema, wanapitia katika kipindi kigumu sana. Nafahamu viongozi wetu wakuu wa chama wakiongozwa naFreeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema taifa, wanakabiliwa na kesi lukuki mahakamani. Nafahamu baadhiya makanda wetu, wamejeruhiwa kwa risasi wakati wauchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni namaeneo mengine.

Nafahamu baadhi ya wanachama wetu, wametekwa nawanaodhaniwa kuwa maharamia ya CCM (Chama Cha Mapinduzi). Nafahamu kuwa aliyekuwa mbunge wetu waSingida Mashariki, Tundu Lissu, alishambuliwa kwa risasi nakuumizwa vibaya na sasa amevuliwa ubunge. Nafahamu.

Lakini napenda kuwahakikishia, kwamba mimi na baadhi yawenzangu, pamoja na vitimbwi vyote hivyo, bado tuko imarana tutaendelea kukulinda chama hiki na kulinda matakwa yawananchi yaliyotokana na uchaguzi mkuu uliyopita, hadi tone letu la mwisho.”

Katika hatua nyingine, mbunge huyo alitumia mkutano wake huo, kutangaza kazi alizozifanya tangu alipochaguliwa kuwambunge wa jimbo hilo, pamoja na miradi aliyoisimamia nakuitekeleza kupitia fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleoya JimboCommunity  Development Catalyst Fund (CDCF).

Alitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa fedha za mfukowajimbo, kuwa ni pamoja na ujenzi wa eneo la kupumzikiawagonjwa na hasa wanawake wanaokwenda kupata hudumaya mama na mtoto, katika zahanati ya Mavulunza, kata yaKimara.

Kwa mujibu wa Kubenea, jengo hilo ambalo limegharimuzaidi ya Sh. 9 milioni, tayari limekamilika na linatumika kwazaidi ya miaka miwili sasa.

Miradi mingine iliyotekelezwa na mfuko wa jimbo, niukarabati wa madarasa na vyumba vya walimu katika shukeya Msingi Mabibo, kata ya Makuburi; ujenzi wa uzio katikashule ya Sekondari Kimara na uchimbaji wa kisima, katikasoko la Mabibo, kata ya Mabibo.

Mbali na miradi hiyo, Kubenea amaetaja mingineiliyotekelezwa, ni ujenzi wa miundo mbinu ya maji katikashule ya Msingi Golani, kata ya Kimara; ujenzi wa kivuko cha waendao kwa miguu, kata ya Mabibo; ukaratabati wa soko la Kapera, lililopo katika kata ya Makurumla.

Ametaja pia ugawaji wa madawati 490 katika shule zote zamsingi na sekondari ndani ya jimbo lake, pamoja na ukarabatina ujenzi wa miundo mbinu katika shule ya Msingi Kawawa, iliyopo kata ya Mabibo; shule ya Sekondari Mashujaa, kata yaSinza na shule ya Msingi Karume, liyopo kata ya Makurumla.

Katika kata ya Manzese, fedha za mfuko wa jimbozinatarajiwa kujenga daraja linalounganisha Sinza naManzese, kusaidia ujenzi wa uzio katika zahanati ya Manzesena kusaidia baadhi ya vikundi vya wajasiriamali vivyopokatika kata hiyo.

Tayari vikundi vya aina hiyo, vilivyopo kata ya Mabibo, vimesaidiwa kwa kupewa pikipiki sita zenye jumla ya Sh. 18 milioni.

Akizungumza katika mkutano huo, mmoja wa wazeewaliohudhuria mkutano huo, Absalom Daniel Mashoto, alimsifu Kubenea kwa hatua yake ya kuita viongozi wake nakuwaeleza kazi alizozifanya.

Alisema, Kubenea amekuwa mbunge wa kwanza waChadema kukutana na aliowaita, “wadau wake wakuu,” nakuwaeleza kazi alizozifanya na anazotarajia kuzifanya katikamuda wake wa ubunge.

Nakupongeza sana kijana wetu. Huu ndio uongozi. Usirudinyuma. Nenda bungeni na ukirudi, fika kwa wananchi wakokuwapa mrejesho wa kile ulichokifanya,” ameeleza Mashoto.

Amesema, ukifanya haya na mengine, siyo tu utakuwaumetimiza wajibu wako kwa wananchi wako waliokuchagua, lakini pia utakuwa umewafanya wale waliokuunga mkonokutembea kifua mbele.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!