Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Pambano la Mwakinyo sasa ni bure
Michezo

Pambano la Mwakinyo sasa ni bure

Spread the love

WAPENZI wa mchezo wa ngumi nchini watepata fulsa ya kushuhudia mpambano wa kimataifa utakaowakutanisha Bondia Hassan Mwakinyo wa Tanzania dhidi ya mpinzani wake kutoka Ufilipino, Arney Tinampay bila kiingilio. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Bondia Mwakinyo amefikia hatua hiyo baada ya kukubaliana na wadhamnini waliojitokeza kudhamini mchezo huo ili waweze kuleta chachu kwa mchezo huo nchini ili uweze kuwanufaisha mabondia wengi ambao wana vipaji.

“Mchezo wa ngumi Tanzania umetupwa sana tofauti na kama ilivyo michezo mingine kama mpira, ningependa kutumia nafasi hii kwa ukubwa huu kusema kuwa pambano langu mimi halitakuwa na viingilio kwa sababu lengo ni kuhamasisha ngumi watu waipende na kuisapoti,” amesema Mwakinyo.

Aidha Mwakinyo alielezea kuwa kama angekuwa anataka kupata hela basi asingepigana Tanzania angeweza kwenda hata nje ya nchi, lakini lengo ni kuhamasisha mchezo ili mabingwa wanaokuja wapate sapoti kama tuliyonayo sisi sasa.

Pambano hilo linategemea kuchezwa siku ya Ijumaa Novemba 27, 2019 kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam majira ya usiku ambapo mchezo utakuwa wa raundi 10.

Mwakinyo kwa sasa ndiye bondia namba moja nchini na barani Afrika kwenye uzito wa kilo 69, huku Tinampay naye akiwa ni bondia namba moja nchini Ufilipino kwenye uzito huo huo wa kilo 69.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!