Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa PAC yabaini ‘madudu’ NIDA, Bil 1 za Tamasha la Utalii
Habari za Siasa

PAC yabaini ‘madudu’ NIDA, Bil 1 za Tamasha la Utalii

Spread the love

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) nchini Tanzania, imebaini upungufu katika maeneo mawili ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na matumizi yasiyozingatia taratibu ya Sh. 1.51 bilioni yaliyofanywa na wizara ya maliasili na utalii. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa tarehe 22 Mei, 2020 na PAC katika taarifa yake kuhusu uchambuzi ilioufanya kuhusu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2019.

Akiwasilisha taarifa hiyo bungeni jijini Dodoma, makamu mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly amebainisha maeneo hayo ni dosari katika utunzaji wa malighafi za kuzalisha vitambulisho vya Taifa zenye thamani ya Sh. 42 bilioni.

Eneo la pili ni kutokuwepo kwa mikataba kati ya NIDA na watumiaji wa taarifa za NIDA hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Amesema, katika dosari ya utunzaji wa malighafi ya vifaa vya kutengeneza vitambulisho vya Taifa, kamati imebaini; kutokuwepo kwa taarifa sahihi za mahitaji ili kubaini mahitaji halisi ya vifaa vya kutengeneza vitambulisho (Poor management of stock levels).

“Uwepo wa malighafi ya ziada ikilinganishwa na mahitaji halisi ya utengenezaji wa vitambulisho vya Taifa ambayo haiwezi kutumika hivi karibuni. Kiasi kilichokuwepo tarehe 30 Juni, 2019 ni vipande 5,411,500 vyenye thamani ya Sh. 42.62 bilioni, kiasi hiki kinaweza kutumika kwa siku 677 sawa na mwaka mmoja na miezi nane kwa uzalishaji wa kadi 8,000 kwa siku,” amesema Hilaly ambaye pia ni Mbunge wa Sumbawanga Mjini

Amesema kamati hiyo imebaini, kukosekana eneo linalofaa kuhifadhia vifaa badala yake vinahifadhiwa chini ya sakafu na kadi zilizoharibika zinahifadhiwa pamoja na ambazo hazijatumika hali inayochangia kuwepo kwa upotevu na ugumu wa kutambua kadi zilizotumika na ambazo bado hazijatumika.

“Eneo la pili ambalo Kamati ilibaini katika NIDA ni kutokuwepo kwa mikataba kati ya NIDA na taasisi zinazotumia taarifa za NIDA. Kifungu 4.9.2 cha Mpango Mkakati (Strategic plan) wa miaka mitano wa NIDA (2019/2020 – 2023/2024) unaitaka NIDA kufanya tathmini ili kuongeza mapato kupitia kuingia hati za makubaliano (MOU) kati yake na taasisi zinazotumia taarifa zake.”

“Uchambuzi kamati umebaini hadi sasa, NIDA wamekuwa wakichangia matumizi ya taarifa zake na taasisi binafsi 41 na 26 za umma kwa matumizi mbalimbali bila ya kuwa na mikataba au hati za makubaliano (MOU),” amesema.

Hilaly amesema, “kutokuwepo mikataba au makubaliano rasmi na watumiaji kutoka taasisi hizo, kunaikosesha Serikali tozo ambayo ingepatikana kutoka kwa watumiaji. Aidha, Serikali inakosa nafasi ya kuchukua hatua kwa watumiaji ikitokea wamekiuka masharti ya matumizi waliyoomba.”

Taarifa hiyo imezungumzia pia matumizi ya Sh. 1.51 bilioni katika wizara ya maliasili na utalii bila ya kuwepo kwenye mpango wa bajeti.

Hilaly amesema, taarifa ya CAG imebainisha wizara ya maliasili na utalii ilikusanya fedha kutoka taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara hiyo kiasi cha Sh.1.51 bilioni kwaajili ya shughuli za Tamasha la Utalii “Utalii Festival”. Tamasha hilo lilifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Manyara na Zanzibar.

Pamoja na nia njema ya wizara katika kukuza utalii kupitia tamasha husika, CAG amefafanua fedha hizo zilitumika bila ya kuwa kwenye mpango wa bajeti ya wizara na pia zilitumika kabla ya kupata vibali husika.”

“Aidha, hoja ya ukaguzi inabainisha kuwa fedha hizo zilitumika bila idhini ya Bunge kama Kanuni za fedha za umma zinavyoelekeza,” amesema Hilaly

Amebainisha matumizi ya fedha hizo kuwa ni; Sh. 479.75 milioni, malipo kwenye kwa taasisi nyinginezo; Sh. 643.46 milioni, malipo kwa wazabuni; Sh. 52.15 milioni, malipo kwa vikundi vya sanaa na wasanii na Sh.135.15 milioni, posho ya kujikimu kwa watumishi wa wizara na kikosi kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!