Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

PAC: BoT inachelewa kuhesabu, kuharibu fedha

Spread the love

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) nchini Tanzania, imesema Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekuwa ikichelewa kuhesabu fedha zinazotoka benki za biashara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea)

PAC imesema hayo kupitia taarifa yake iliyosomwa leo Ijumaa tarehe 22 Mei, 2020 na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hilaly alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo, kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2019.

Hilaly amesema, kwa taarifa ya ukaguzi ya mwaka 2019, kamati ilichambua taarifa ya hesabu za BoT na kubaini eneo moja ambalo benki hiyo inatakiwa kulifanyia kazi kwa msisitizo.

“Eneo hilo linahusu BoT kuchukua muda mrefu kuhesabu fedha zinazotoka kwenye benki za biashara,” amesema Hilaly.

“Kwa mwaka huu hadi ukaguzi unakamilika CAG, alibaini zaidi ya Sh. 300 bilioni zilikuwa zinahusika katika hoja hii.”

Makamu huyo mwenyekiti amesema, “taarifa ya CAG ilibainisha pia, BoT inachukua muda mrefu katika kuharibu fedha chakavu zinazotoka kwenye mzunguko.”

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) nchini Tanzania, imesema Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekuwa ikichelewa kuhesabu fedha zinazotoka benki za biashara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea) PAC imesema hayo kupitia taarifa yake iliyosomwa leo Ijumaa tarehe 22 Mei, 2020 na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hilaly alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo, kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2019. Hilaly amesema, kwa taarifa ya ukaguzi ya mwaka 2019, kamati ilichambua taarifa ya hesabu za BoT na kubaini eneo moja ambalo benki hiyo inatakiwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!