Ofisa TRA, wenzake 17 wa CCM mbaroni tuhuma za rushwa

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mtwara, imewakamata wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 18 akiwamo Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Muhaji Mrope anayetaka kuwania ubunge jimbo la Ndanda, wakituhumiwa “kutoa rushwa na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu kabla ya wakati.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara…(endelea)

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo, akizungumza na MwanaHALISI ONLINE leo Jumanne tarehe 2 Juni 2020 amesema, watuhumiwa hao waliwakamata jana Jumatatu.

Amesema, kati yao 16 waliwaachia jana hiyohiyo baada ya mahojiano na wawiki akiwamo Mrope wameachiwa leo Jumanne kwa dhamana wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Ngailo amesema, jana walipokea taarifa kutoka, “kwa msiri wetu, ikielezea leo (jana) tarehe 01 Juni 2020 kunafanyika vikao viwili, cha kwanza kimefanyika nyumbani kwa katibu mwenezi wa CCM kata ya Mlingula muda wa saa 3:00 asubuhi na kingine kinafanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa CCM tawi la Mlingula saa 5:00 asubuhi.”

“Taarifa hiyo ilieleza vikao vyote hivyo, vimefanyika kwa lengo la kuwashawishi wajumbe watakaopiga kura za maoni kuwachagua wagombea ubunge Jimbo la Ndanda Wilaya ya Masasi,” amesema Ngailo

Ngailo amesema, “taarifa inaeleza, viongozi hao wa CCM kwa maana ya katibu mwenezi CCM kata ya Mlingula, Martine Chinemba na mwenyekiti wa CCM tawi la Mlingula, Hussein Bwanali ni mawakala ambao wanatumiwa na mwanachama wa CCM ambae pia ni Afisa wa TRA Mkoa wa Dar es Salaam, Muhaji Mrope aliyeonesha nia ya kugombea ubunge Jimbo la Ndanda kwenye uchaguzi ujao.”

Akizungumzia jinsi walivyowakamata, Ngailo amesema, baada ya kupokea taarifa hiyo, maafisa wa Takukuru, Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, waliweza kufika eneo la tukio ambapo ni nyumbani kwa Bwanali maarufu ‘DJ’ mtaa wa Tandika kata ya Mlingula.

Amesema, maafisa hao, walifanikiwa kuwakuta Mrope, mawakala wake pamoja na wajumbe wakiwa katika kikao hicho na kuweza kuwaweka chini ya ulinzi watu wote 18 na kuwafikisha katika ofisi za Takukuru, Wilaya ya Masasi kwa mahojiano.

“Baada ya mahojiano watuhumiwa 16 ambao walikua ni wanachama, wajumbe na baadhi ya viongozi waliachiwa kwa dhamana jana na watuhumiwa wengine ambao ni Muhaji Mrope na Chinemba walihifadhiwa mahabusu katika kituo cha Polisi Wilaya ya Masasi wakati uchunguzi ukiendelea na kuachiliwa leo kwa dhamana,” amesema

Amesema, wanaendelea na uchunguzi ili kujua hatua zaidi za kufuata.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mtwara, imewakamata wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 18 akiwamo Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Muhaji Mrope anayetaka kuwania ubunge jimbo la Ndanda, wakituhumiwa “kutoa rushwa na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu kabla ya wakati.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara…(endelea) Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo, akizungumza na MwanaHALISI ONLINE leo Jumanne tarehe 2 Juni 2020 amesema, watuhumiwa hao waliwakamata jana Jumatatu. Amesema, kati yao 16 waliwaachia jana hiyohiyo baada ya mahojiano na wawiki akiwamo Mrope wameachiwa leo Jumanne kwa dhamana wakati uchunguzi zaidi ukiendelea. Ngailo amesema,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!