Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Odinga na Kenyatta kuzipiga tena Oktoba 17 
Makala & Uchambuzi

Odinga na Kenyatta kuzipiga tena Oktoba 17 

Uhuru Kenyatta (kulia) na Raila Odinga
Spread the love

WAFULA Chebukati, Mwenyekiti  wa  Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC), ametangaza tarehe mpya ya kurudia uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 17 Oktoba 2017, anaandika Mwandishi wetu.

Tarehe hii imepangwa kutokana na maelekezo ya Mahakama Kuu ya Kenya yaliyotolewa siku ya Ijumaa iliyopita.

Uchaguzi huu hautakuwa na uteuzi wa wagombea wa nafasi ya urais. Chebuka akitangaza tarehe hiyo jana alisema kuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga na mgombea mwenza Kalonzo Musyoka na Rais

Uhuru Kenyata na mgombea mwenza wake William Ruto ndio watakuwa wagombea pekee.
“Tume inapitia upya mahitaji ya uendeshaji na utaratibu wa kufanya uchaguzi mpya na itashirikisha wadau baadaye,” Chebukati alisema wakati akitangaza tarehe hiyo mpya.

Chebukati alisema kuwa kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama ya Juu, ni muhimu kupata hukumu kamili ili kuruhusu tume ya uchaguzi kufahamu maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa katika usimamizi wa uchaguzi mpya. “Tume inaomba  muwe wavumilivu, muwe  waelewa ili tuweze kushirikiana na kufanya uchaguzi huru, wa haki, wa kuaminika na wa amani,” alisema.

Mahakama Kuu ya Kenya tarehe 1 Septemba ilitangaza kufanyika kwa  uchaguzi mpya ndani ya siku 60 baada ya kugundua kuwa taratibu hazikufuatwa  katika uchaguzi mpya wa mwezi uliopita. Mahakama hiyo iliamua kwamba uchaguzi wa rais haukufanyika kwa mujibu wa katiba, na hivyo kupelekea kutoa matokeo batili, na kusema Kenyata hakuchaguliwa kwa usahihi.

Waamuzi majaji wanne kati ya sita katika Mahakama Kuu ya Kenya walihukumu kwa kukubaliana na madai ya  Odinga mgombea wa nafasi ya Urais kutoka chama cha National Super Alliance (NASA) kilichopinga matokeo ya uchaguzi na kufungua ombi kwa mahakama hiyo ya juu.

Wachambuzi wanasema utenguaji wa ushindi wa Kenyatta ni muhimu sana kwa Odinga kama karata yake ya mwisho ya kugombea kiti cha urais kwani ametamka uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa mwisho kwake na kuwa asingegombea tena nafasi hiyo ya juu.

Hii ni mara ya nne kwa Odinga(72) kushindwa uchaguzi kwa nafasi ya urais, na mara zote amekuwa akilalamika kuwa uchaguzi ulikiuka taratibu. Kwa mara ya kwanza Mahakama ya Juu siku ya Ijumaa ilikubaliana na  madai yake. Hata hivyo Kenyatta, aliyepata kura milioni 8.22 dhidi ya Odinga aliyepata kura milioni 6.8, (tofauti ya kura milioni 1.42)  alisema kushinda kwake kumetokana na  ‘mapenzi ya watu.’

“Ni muhimu kuheshimu utawala wa sheria, tunaamini  katika utawala wa sheria.  Tuko tayari kurudi tena kwa watu kwa ajenda ileile,” alisema. Aliwataka wakenya kudumisha amani huku akiapa kumshinda  mpinzani wake Odinga na NASA katika uchaguzi wa marudio. Wakati huo huo Odinga amesisitiza nchi nyingine za Kiafrika  kufuata kilichotokea Kenya kwa kuheshimu demokrasia katika uendeshaji wa serikali.

Nchi za Uganda, Ghana, Zimbabwe, Zambia, Nigeria na Sierra Leone ni nchi nyingine katika bara la Afrika ambako uchaguzi wa rais umewahi kupingwa  katika mahakama hata hivyo hukumu haikuweza kubatilisha matokeo ya urais

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!