Donald Trump, Rais wa Marekani

Obama amnaga Trump, Ikulu yamtetea

Spread the love

BARACK Obama, Rais Mstaafu wa Marekani, amemtuhumu rais wa sasa Donald Trump kwamba ameshindwa kuukabili ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Kupitia kituo cha Televisheni cha CNN, Obama ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waiokuwa wafanyakazi wake wa Ikulu, sambamba na timu ya kampeni ya uchaguzi ya Joe Biden.

Amesema, mbinu anazotumia Trump kukabiliana na janga la corona katika taifa hilo, hazijasaidia chochote na kwamba, yeye (Trump) ni mwingoni mwa watu wanaopaswa kulaumiwa kwa vifo vingi vilivyotokea.

Mpaka tarehe 9 Mei 2020, Marekani kumetokea vifo vya watu zaidi ya 77,000 vilivyotokana na corona. Maambukizi yamefikia watu zaidi ya milioni 1.2.

Obama amesema, takwimu hizo zimeweka rekodi ya juu kabisa katika uso wa dunia kutokana na Trump kushindwa kujua namna ya kuwaokoa Wamarekani kutokana na janga hilo.

Trump aliahidi kwamba, mpaka mwezi Februari mwaka huu, ugonjwa huo ungekuwa umemalizwa kabisha ndani ya mipaka ya taifa hilo.

Hata hivyo, ilivpofika katikati ya Machi, Trump alieleza kwamba ugonjwa huo umekuwa ukisambaa kwa kiwango cha juu ndani ya taifa hilo.

Ilipofika Aprili, Trump alidai dawa za kuua bakteria zinaweza kuzuia virusi, hata hivyo wanasayansi ndani ya taifa hilo walilikana kwamba si kweli.

Kutokana na kuchanganyikiwa na kasi ya maambukizi, wiki iliyopita Trump aliahidi atavunja kikosi kazi kinachopambana na kusambaa kwa virusi vya corona, baadaye akatangaza kuachana na mpango huo.

Ikulu ya Marekani imemtetea Trump kwamba amekuwa akifanya kazi kubwa kuhakikisha anakabiliana na corona na kwamba, ameliokoa taifa hilo kutumbukia katika janga kubwa.

BARACK Obama, Rais Mstaafu wa Marekani, amemtuhumu rais wa sasa Donald Trump kwamba ameshindwa kuukabili ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea). Kupitia kituo cha Televisheni cha CNN, Obama ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waiokuwa wafanyakazi wake wa Ikulu, sambamba na timu ya kampeni ya uchaguzi ya Joe Biden. Amesema, mbinu anazotumia Trump kukabiliana na janga la corona katika taifa hilo, hazijasaidia chochote na kwamba, yeye (Trump) ni mwingoni mwa watu wanaopaswa kulaumiwa kwa vifo vingi vilivyotokea. Mpaka tarehe 9 Mei 2020, Marekani kumetokea vifo vya watu zaidi ya 77,000 vilivyotokana…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!