Ninja arejea Yanga

Spread the love

ABDALLAH  Shaibu (Ninja) amerejea tena ndani ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya La Garaxy inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezaji huyo amesaini mkataba huo mapema hii leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo chini ya makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Frederick Mwakalebela na kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Patrick Simon.

Beki huyo hapo awali alijiunga na Yanga 2017 akitokea Zanzibar kwa mkataba wa miaka miwili, na kufanikiwa kucheza Yanga kwa mafanikio makubwa na mwisho wa msimu alijiunga na klabu ya La Garaxy na baadae kupelekwa kwa mkopo kwenye timu ya MFK Vyskov.

Yanga kwa sasa inaendelea kuimalisha kikosi chake ambapo mpaka sasa imeshasajili jumla ya wachezaji watano ambao ni Zawadi Mauya, Bakari Mwamnyeto, Wazir Junior, Yassin Mustapha na Ninja.

ABDALLAH  Shaibu (Ninja) amerejea tena ndani ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya La Garaxy inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). Mchezaji huyo amesaini mkataba huo mapema hii leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo chini ya makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Frederick Mwakalebela na kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Patrick Simon. Beki huyo hapo awali alijiunga na Yanga 2017 akitokea Zanzibar kwa mkataba wa miaka miwili, na kufanikiwa kucheza Yanga kwa mafanikio makubwa na mwisho wa msimu alijiunga na klabu ya La Garaxy na baadae kupelekwa kwa mkopo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

One comment

  1. jackson Tagagasi

    NINJA KARIBU KWA WANANCHI UPIGE SOCCER

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!