Watu wasiojulikana wafungua matairi gari la Lema

MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema watu wasiojulikana walifungua baadhi ya nati kwenye taili ya gari yake kitu ambacho kingeweza kumsababishia ajali, anaandika Hamis Mguta.

Lema na Mbunge wa Arumeru mashariki (Chadema), Joshua Nassari walipanga kuondoka na gari hilo jana usiku kuelekea Dar es Salaam kuwasilisha ushahidi wa tuhuma za rushwa za madiwani waliohama Chadema ambapo kabla ya kuanza safari walibaini kuwapo kwa tatizo kwenye gari.

“Juzi nilisikia sauti isiyosawa tairi za nyuma nikapaki gari Equator Hotel. Dereva alipochukua gari tairi zote zikachomoka. Ninalindwa na Mungu.

“Tulibaini tairi za mbele wamefungua wakaacha wheelnut mbili mbili kila tairi, nyuma waliacha moja upande wa kushoto na kulia wakaacha mbili,” aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Amesema kuwa baada ya kuhisi tatizo hilo aliliegesha katika hoteli ya Equator na baadaye kuomba msaada kwenye gari la Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph kwenda naye Dar es Salaam.

“Asubuhi leo (Jumatatu) nikamtuma dereva wangu akachukue gari Equator hoteli alipeleke gereji na baada ya kutoka mita chache tairi zilichomoka,” amesema.

Amesema tayari amemuagiza dereva kwenda kutoa taarifa polisi lakini ameiomba kampuni ya ulinzi ya Inteligence inayolinda nyumba yake kufanya uchunguzi kubaini watu walioingia ndani na kufungua nati.

MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema watu wasiojulikana walifungua baadhi ya nati kwenye taili ya gari yake kitu ambacho kingeweza kumsababishia ajali, anaandika Hamis Mguta. Lema na Mbunge wa Arumeru mashariki (Chadema), Joshua Nassari walipanga kuondoka na gari hilo jana usiku kuelekea Dar es Salaam kuwasilisha ushahidi wa tuhuma za rushwa za madiwani waliohama Chadema ambapo kabla ya kuanza safari walibaini kuwapo kwa tatizo kwenye gari. “Juzi nilisikia sauti isiyosawa tairi za nyuma nikapaki gari Equator Hotel. Dereva alipochukua gari tairi zote zikachomoka. Ninalindwa na Mungu. “Tulibaini tairi za mbele wamefungua wakaacha wheelnut mbili mbili kila tairi, nyuma waliacha moja…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Hamisi Mguta

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube