Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Ni vituko: Fomu zatolewa usiku, zarejeshwa usiku
Tangulizi

Ni vituko: Fomu zatolewa usiku, zarejeshwa usiku

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

HOFU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuanguka vibaya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, imetamalaki. Anaripoti Martin Kamote…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na John Marema, Mkurugenzi wa Itikadi na Uenezi na Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 31 Oktoba 2019.

“Mbeya Mjini, Kata za Iyunga jana (tarehe 30 Oktoba 2019) kutwa mzima wasimamizi wamefunga ofisi,” amedai Mrema na kuongeza “Kule Liwale, wagombea wa CCM wanapewa fumo usiku, wanajaza na kurejesha usiku halafu mchana ofisi za wasimamizi hazifunguliwi.”

Akieleza masikitiko yake Mrema amedai, hujuma hizo pia zimefanywa mkoani Ruvuma ambapo kwenye Kata ya Chipata, mtendaji amegoma kutoa fomu kwa madai anaumwa jino.

Amesema, licha ya kuwa leo ni siku ya tatu tangu kuanza kutolewa kwa fomu za kugombea, baadhi ya ofisi hazijafunguliwa.

“Ofisi za wasimamizi zimefungwa siku ya tatu leo, wagombea wetu Liwale, Tunduru wanahaha kwenye ofisi hizo kutaka fomu, mpaka sasa hawajafanikiwa,” amesema.

Amedai, hujuma nyingine wanaofanyiwa upinzani ni pamoja na wagombea kukamatwa kabla ya kurejesha fomu ya kugombea.

“Wagombea wetu wa Vyawa katika Kata za Hasanga, huko Ruvuma pia Iwili na Malangai, waliokuwa wakiwasubiri wasimamizi wa kata wafungue ofisi, wamewakamata pale pale bila kuwapa sababu,” amesema na kuongeza;

“Wagombea wetu wanakumbana na kikwazo hicho, haya yote hayafanywi kwa bahati mbaya. Mkoa wa Kagera na Ukerewe kuna watu wanafoji barua za Chadema ilimradi kuhujumu kwamba wagombea wetu wamechukua fomu.”

Akizungumzia Bukoba Vijiji, amesema Kata ya Nyakato wagombea wao ambao walikuwa wakihudumu kwenye Mfuko wa Tasaf, wamepewa vitisho na kulazimisha kutorudisha fumo, vinginevyo watawaondoa kwenye mfuko huyo.

Mrema amedai, mkoani Misingwi katika Kata ya Koromije na vitongoji vyake vyote, wagombea wa Chadema wameambiwa fomu zimekwisha.

“Huko Bukombe ni mwendo wa hujuma tu, wagombe wetu huko wameambiwa hakuna mihuri ya uchaguzi, sasa unawezaje kupokea fomu isiyo na muhuri, je wakiikataa wakati wa kurudisha?” amehoji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!