Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ni ‘nyodo’ za Sugu, Dk Tulia
Habari za Siasa

Ni ‘nyodo’ za Sugu, Dk Tulia

Spread the love

JOSEPH Mbilinyi maarufu ‘Sugu,’ mgombea ubunge Mbeya Mjini (Chadema) na Dk. Tulia Akson, mgombea jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza kutambiana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Wakati Sugu akijigamba kwamba, ‘sasa hivi namfukuza mwizi kimyakimya,’ Dk. Tulia anasema ‘tayari njia nyeupeeee!’ kwenye jimbo hilo.

Wawili hao walitoa majigambo muda mfupi baada ya kurejesha fomu za kugombea ubunge jana tarehe 25 Agosti 2020, kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Elias Ng’wanidako.

Jimbo la Mbeya Mjini ni moja ya majimbo magumu na yenye usindani mkubwa nchini kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Dk. Tulia na Sugu walipishana kwa dakika 50, wakati Sugu akiingia kwenye ofisi hizo saa 4:20, Dk. Tulia aliingia kwenye ofisi hizo saa 5:10.

Dk. Tulia Ackson

“Leo (jana) sijaja na mtiti hapa, tunabadili mbinu kidogo lakini mwendo ni ule ule, nimeamua kuja kimya kimya kama namfukuza mwizi vile ila shughuli ni pale tarehe 5 Sepetmba Lissu (Tundu Lissu, mgombea urais kupitia chama hicho) atakapokanyaga ardhi ya Mbeya.”

“Muda wa maandamano utafika, lakini tunaanza kwa staili hii. Staili ya kuchukua fomu safasi hii ni tofauti na ile ya 2015, safari hii kimya kimya ila salam zimewafikia,” amesema Sugu.

Sugu alifika kwenye viunga vya ofisi hizo akiwa na gari yake ndogo aina ya Toyota IST, nyeusi akiwa na watu wengine wanne, viongozi wa chama hicho Mbeya.

Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha

Kwa upande wake, Dk. Tulia amesema, ni wakati kwa CCM kurejesha jimbo hilo kwenye himaya yake na kuwa, yeye ndio atayelinyakua kutoka mikononi mwa Sugu aliyehudumia jimbo hilo kwa miaka 10.

“CCM imejipanga vizuri zaidi na nina uhakika, safari hii jimbo linarejea kwetu,” amesema Dk. Tulia huku akisisitiza kwamba kila chama kimejipanga lakini sio zaidi ya CCM.

Dk. Tulia ambaye alikuwa Naibu Spika kaika Bunge la 11 lililoongozwa na Spika Job Ndugai, alifika kwenye ofisi hizo akiwa na magari manne, moja likiwa la polisi waliosindikiza msafara wake.

Sugu na Dk. Tulia ni miongoni mwa wagombea wa jimbo hilo walioteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kugombea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!