‘Ni kweli Lipumba anatumika’ – MwanaHALISI Online
Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)
Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)

‘Ni kweli Lipumba anatumika’

HUWEZI kuamini kwa kusikia kwamba Jeshi la Polisi hutumika kutekeleza
matakwa ya watawala dhidi ya haki ya wananchi, anaandika Jabir Idrissa.

Picha ifuatayo, itakusaidia kuamua iwapo ni kweli unachokisikia kuwa Serikali ya CCM kupitia Polisi, ndio inambeba Profesa Ibrahim Lipumba katika mgogoro wa uongozi anaoshutumiwa kuuanzisha ndani ya Chama chaWananchi (CUF).

Mwanzoni mwa wiki, Prof. Lipumba, aliyejiuzulu uenyekiti kwa hiari yake 6 Agosti mwaka jana, akisingizia ujio wa Edward Lowassa kwenye kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuelekea uchaguzi mkuu, alizuru Mkoa wa Mtwara.

Katika ziara yake hiyo akijitambulisha kuwa ni mwenyekiti halali wa CUF, alifika Mtwara mjini na Wilaya ya Newala. Mote humo alifanikiwa kufanya vikao vya ndani na waliotajwa kuwa wanachama na viongozi wa ngazi ya wilaya wa chama hicho.

Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma, ndiye aliyemsaidia Prof. Lipumba kufanikisha ziara yake ya kwanza tangu alipojichimbia kwenye Ofisi Kuu za CUF, Buguruni, Dar es Salaam baada ya kutambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Kwa hivyo, kupitia msaada wa mbunge Nachuma, Prof. Lipumba amefanikiwa kufanya ziara hiyo. Siri kubwa ni kwamba wakati wa safari yake hiyo, nyuma, mbele na pembeni, analindwa na askari wa Jeshi la Polisi.

Polisi ndio wanaompa ulinzi makini Prof. Lipumba, ambaye kulingana na vikao halali vya juu vya CUF, ameshafukuzwa uanachama wa chama hicho tangu 27 Septemba mwaka huu, kupitia azimio la Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT).

Jana, mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed Katani, amelalalamikia Polisi wa Mkoa wa Mtwara kuvuruga kikao chake na viongozi wa Wilaya ya Newala, ilhali alikuwa na ruhusa ya jeshi hilohilo.

Katani ambaye mwezi uliopita aliteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi kuwa mjumbe katika Kamati ya Uongozi ya chama hicho

HUWEZI kuamini kwa kusikia kwamba Jeshi la Polisi hutumika kutekeleza matakwa ya watawala dhidi ya haki ya wananchi, anaandika Jabir Idrissa. Picha ifuatayo, itakusaidia kuamua iwapo ni kweli unachokisikia kuwa Serikali ya CCM kupitia Polisi, ndio inambeba Profesa Ibrahim Lipumba katika mgogoro wa uongozi anaoshutumiwa kuuanzisha ndani ya Chama chaWananchi (CUF). Mwanzoni mwa wiki, Prof. Lipumba, aliyejiuzulu uenyekiti kwa hiari yake 6 Agosti mwaka jana, akisingizia ujio wa Edward Lowassa kwenye kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuelekea uchaguzi mkuu, alizuru Mkoa wa Mtwara. Katika ziara yake hiyo akijitambulisha kuwa ni mwenyekiti halali wa CUF, alifika Mtwara mjini na Wilaya ya Newala. Mote humo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Jabir Idrissa

+255 774 226248
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube