Willium Ngereja (katikati)

Ngeleja, Bukwimba, Maige na Kalanga wapigwa

Spread the love

WABUNGE wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kura za maoni za. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea)

Wabunge hao wameshindwa katika kura za maoni zilizofanyika leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020 ikiwa ni mwendelezo wa wabunge kuanguka kwenye kura hizo.

Jimbo la Sengerema Mkoa wa Mwanza, mbunge anayemaliza muda wake, William Ngeleja ameshindwa kwa kupata kura 120 dhidi ya Hamisi Tabasamu aliyeongoza kwa kura 335.

Wagombea walikuwa 60 huku wajumbe waliohudhuria mkutano huo wakiwa 929.

Katika Jimbo la Msalala Mkoa wa Shinyanga, Ezekiel Maige amepata kura 118 dhidi ya mshindi Iddi Kassim aliyepata kura 327. Khatib Mgeja amekuwa wa tatu akipata kura 75.

         Soma zaidi:- 

Mbunge anayemaliza muda wake wa Busanda Mkoa wa Geita, Lolencia Bukwimba ameshindwa kura za maoni kwa kupata kura 94 dhidi ya Masunga Kulwa Biteko, ambaye ni pacha wa Doto Biteko, waziri wa Madini aliyepata kura 665

Fredrick, mtoto wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameongoza kura za maoni jimbo la Monduli Mkoa wa Arusha kwa kura 244 dhidi ya Mbunge anayemaliza muda wake, Julius Kalanga aliyepata kura 162 na Wilson Lengima ameshika nafasi ya tatu kura 149.

Wakati huo huo, Afisa Tawala Tume ya Madini, Saashisha Mafuwe ameongoza kura za maoni kupitia CCM Jimbo la Hai Mkoa wa Kilimanjaro kwa kupata kura 124 kati ya 452 wa pili ni Fuya Kimbita aliyepata kura 85 na Abubakari Msangi akishika nafasi ya tatu kura 48

Pia, Profesa Patrick Ndakidemi ameongoza kura za maoni kupitia CCM jimbo la Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro akipata kura 262 kati ya 594. Deogratius Mushi amekuwa wa pili akipata kura 42 na watatu ni Moris Makoi kura 35

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

WABUNGE wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kura za maoni za. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea) Wabunge hao wameshindwa katika kura za maoni zilizofanyika leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020 ikiwa ni mwendelezo wa wabunge kuanguka kwenye kura hizo. Jimbo la Sengerema Mkoa wa Mwanza, mbunge anayemaliza muda wake, William Ngeleja ameshindwa kwa kupata kura 120 dhidi ya Hamisi Tabasamu aliyeongoza kwa kura 335. Wagombea walikuwa 60 huku wajumbe waliohudhuria mkutano huo wakiwa 929. Katika Jimbo la Msalala Mkoa wa Shinyanga, Ezekiel Maige amepata kura 118 dhidi ya mshindi Iddi Kassim aliyepata kura 327. Khatib Mgeja amekuwa wa tatu akipata…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

One comment

  1. Hao wanaotangatanga ni kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Kama kuwatumikia wananchi ilitosha kabisa walikoku
    wa.Nawapongeza CCM kwa kuliona hilo.Wanajua nani ni mtu makini na yule anaejipendekeza.Aidha nawapongeza wapinzani wasioyumba na hakika bila utani nawaambia CCM wanawapenda mno kuwachemsha kwani mnaifanya serkali iamke pale inaposhindwa kumtumikia vema mwananchi.Unganeni mpate ngome imara.Msijali kejeli za kisiasa.Nyuzi moja ya katani ni dhaifu mno lakini
    zikiungana nyingi zinanyonga simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!