Neymar, wenzake wakumbwa na corona

Spread the love

NEYMAR de Santos, mshambuliaji wa timu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya nchini Ufaransa na wachezaji watatu wa timu hiyo, amekutwa na virusi vya corona. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Licha ya kalbu hiyo kutotaja majina ya wachezaji wengine waliokumbwa na ugonjwa huo sambamba na Neymar, taarifa kutoka klabuni hapo zinaeleza wanaotajwa kukumbwa na corona ni pamoja na Angel Di Maria (32) na Leandro Paredes (26).

PSG kwenye Ligi Kuu ya taifa hilo, ni mabingwa watetezi ambapo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, wameshika nafasi ya pili.

Taarifa za wachezaji hao kukumbwa na corona, zimethibitishwa na taarifa ya klabu hiyo iliyowekwa kwenye mitandao yao ya kijamii.

Neymar na wenzake, kwa sasa wamewekwa karantini kwa siku 14 wakiendelea na matibabu. Ligi Kuu nchini humo tayari imeanza kuchezwa.

NEYMAR de Santos, mshambuliaji wa timu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya nchini Ufaransa na wachezaji watatu wa timu hiyo, amekutwa na virusi vya corona. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa ... (endelea). Licha ya kalbu hiyo kutotaja majina ya wachezaji wengine waliokumbwa na ugonjwa huo sambamba na Neymar, taarifa kutoka klabuni hapo zinaeleza wanaotajwa kukumbwa na corona ni pamoja na Angel Di Maria (32) na Leandro Paredes (26). PSG kwenye Ligi Kuu ya taifa hilo, ni mabingwa watetezi ambapo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, wameshika nafasi ya pili. Taarifa za wachezaji hao kukumbwa na corona, zimethibitishwa na taarifa ya…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!