Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera

NEC yatangaza uchaguzi kata 3 

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC), imeitisha uchaguzi mdogo katika kata tatu zilizoshindwa kushiriki uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, kutokana na sababu mbalimbali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kata hizo ni, Nyahanga iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, Igumbilo (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa) na Kibosho Kati (Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro).

Taarifa ya kuitishwa kwa uchaguzi huo mdogo imetolewa kwa umma jana Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020 na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Gerald Mwanilwa.

Taarifa ya Mwanilwa imesema kuwa, uchaguzi huo mdogo utafanyika tarehe 8 Disemba 2020 ambapo kampeni zake zitafanyika kwa siku 21 kuanzia tarehe 17 Novemba hadi Disemba 7 mwaka huu.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema Kata ya Kibosho Kati haitafanya kampeni kwa kuwa wagombea wake walishafanya. Kata hiyo haikufanya uchaguzi kutokana na kukosewa kwa karatasi za kura.

Taarifa ya Mwanilwa imesema, uteuzi wa wagombea kwa vyama ambavyo wagombea wake walifariki dunia katika Kata ya Igumbilo na Nyahanga utafanyika tarehe 16 Novemba 2020.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tume imepanga tarehe 16 Novemba 2020 kuwa ni tarehe ya uteuzi wa wagombea wa vyama ambavyo wagombea wake walifariki kwenye Kata ya Nyahanga na Igumbilo,” imeeleza taarifa hiyo.

NEC imevitaka vyama vya siasa, wagombea pamoja na watendaji wa uchaguzi kufuata sheria na kanuni na maelekezo yake ili chaguzi hizo zifanyike kwa weledi.

“Tume inachukua fursa hii kuwahamasisha watendaji wa uchaguzi kwenye kata hizo kufanya kazi kwa weledi, kwa kuzingatua sheria, kanuni na maelekezo ya tume,” imeeleza taarifa ya Mwanilwa.

Taarifa hiyo imeeleza, tume inavikumbusha vyama vya siasa na wagombea kuhakikisha wanafuata utaratibu wa kisheria kuweka mawakala kwenye vituo vyote vya kupigia kura ili kuhakikisha kwamba maslahi ya wagombea yanalindwa.”

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC), imeitisha uchaguzi mdogo katika kata tatu zilizoshindwa kushiriki uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, kutokana na sababu mbalimbali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam ... (endelea). Kata hizo ni, Nyahanga iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, Igumbilo (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa) na Kibosho Kati (Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro). Taarifa ya kuitishwa kwa uchaguzi huo mdogo imetolewa kwa umma jana Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020 na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Gerald Mwanilwa. Taarifa ya Mwanilwa imesema kuwa, uchaguzi huo mdogo utafanyika tarehe 8 Disemba 2020…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!