Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yaongeza siku za uandikishaji
Habari za Siasa

NEC yaongeza siku za uandikishaji

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeongeza siku tatu katika Zoezi la Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura katika mkoa wa Dar es Salaam, lililotakiwa kukoma leo tarehe 20 Februari 2020. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Dk. Wilson Mahela, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya tume hiyo kufanya tathimini ya zoezi hilo, na kubaini kwamba kuna uhitaji wa siku kuongezeka.

Amesema, zoezi hilo lililoanza tarehe 14 Februari mwaka huu litakoma rasmi tarehe 23 Februari 2020, na kwamba baada ya siku hizo kuisha, muda hautaongezwa tena.

“NEC katika kikao chake kilichofanyika jana tarehe 19 Februari 2020 ilifanya tathimini ya zoezi la uboreshaji  daftari la wapiga kura linaloendelea Dar es Salaam, kwa kutumia  mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 15 kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.

Tume imemua na kuelekeza kuwa,  muda wa zoezi hilo liongezwe kwa siku tatu. Sasa litakamilika tarehe 23 , zoezi la litanedelea hadi siku ya Jumapili katika vituo vyote vya Dar es Salaam, vituo vitendelea kufunguliwa saa 2 asubuhi na kufunguliwa saa 12 jioni,” amesema Dk. Mahela.

Dk. Mahela amesihi wakazi wa Dar es Salaam kutumia vyema ongezeko la siku hizo, ili kuhakikisha wanahuisha taarifa zao katika daftari hilo, kwa ajili ya kupata fursa ya kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.

“Tume inawasishi wananchi wa Dar es Salaam kutumia muda huu vizuri uliongezwa ili kuhakikisha taarifa zao zinaingizwa katika daftari,  kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza katika awamu ya kwanza ya uboreshaji daftari, watumie nafasi hii vizuri wajitokeze kwa wingi. Kadi yako ni kura yako nenda kajiandikishe,” amesema Dk. Mahela.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!