Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera

NEC yaongeza siku mbili kuapisha mawakala

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imeongeza siku mbili zaidi za kuapisha mawakala wa vyama vya siasa watakaosimamia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema, tume imeongeza muda huo kuanzia leo hadi 23 Oktoba 2020.

“Tume imeamua hivyo baada ya kubaini baadhi ya maeneo kuna changamoto ya kufikika kutokana na jiografia,” amesema Dk. Mahera

Shughuli ya uapishaji mawakala ilikuwa ifanyike kwa siku moja ya leo Jumatano lakini tangu asubuhi katika maeneo mbalimbali, kumekuwapo na taarifa kutoka kwa vyama vya siasa na wagombea kulalamikia mawakala wao kutoapishwa.

Hata hivyo, Dk. Mahera amesema, watakaoapishwa katika kipindi hicho ni yale majina yaliyowasilishwa na vyama yakiwa na majina yenye namba za simu na yaliyopangwa kwa kila wakala atasimamia eneo gani.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

“Orodha hiyo imewapanga katika maeneo na huyo wakala anapaswa kuweka namba ya simu na eneo atakalosimamia, usipoweka unaweza kupata shida,” amesema Dk. Mahera

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameandika katika ukurasa wake wa Twitter, “mawakala wetu sehemu mbalimbali nchini, wamezuiwa kuapa mpaka sasa.”

“Arusha mawakala wetu wako kituoni toka asubuhi. tume msicheze na uchaguzi kwani kucheza na uchaguzi ni kuhatarisha usalama wa nchi. Apisheni mawakala wetu na wa vyama vingine vya upinzani tafadhali,” amesema Zitto ambaye pia ni mgombea ubunge Kigoma Mjini

Alichokisema Zitto, kinafanana na kile alichokizungumza mchana wa leo Jumatano, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika wakati anazungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mnyika alisema, katika maeneo mbalimbali kumekuwapo na changamoto ya mawakala wao kuapishwa hivyo kuitaka tume kuwa makini wasije kuharibu uchaguzi huo.

“Tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ikifika jioni ya leo kama mawakala wetu hawajaapishwa basi itangaze tarehe ya nyongeza ya kuwaapisha mawakala wetu,” alisema Mnyika

“Chato kuna kituko, msimamizi wa uchaguzi ameandika barua kusema eti kata mbalimbali za Chato amebaini saini ya katibu wa chama imeghushiwa.”

“Katibu wetu wa chama amethibitisha kwa polisi saini ni ya kwake na anawatambua mawakala, msimamizi wa uchaguzi anasema kuthibitisha saini ni suala la polisi na anasubiri maelezo ya polisi na hadi sasa hawajaeleza lolote,” alisema.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imeongeza siku mbili zaidi za kuapisha mawakala wa vyama vya siasa watakaosimamia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema, tume imeongeza muda huo kuanzia leo hadi 23 Oktoba 2020. “Tume imeamua hivyo baada ya kubaini baadhi ya maeneo kuna changamoto ya kufikika kutokana na jiografia,” amesema Dk. Mahera Shughuli ya uapishaji mawakala ilikuwa ifanyike kwa siku moja ya leo Jumatano lakini tangu asubuhi katika maeneo mbalimbali, kumekuwapo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!