TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imesema, zabuni ya kumpata mchapishaji wa karatasi za kupigia kura ilitangaza kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi wa Umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Dk. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu tarehe 12 Oktoba 2020 amesema, zabuni hiyo ilitangazwa katika tovuti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Gazeti la Serikali la Daily News.
Dk. Mahera amesema, baada ya kutangazwa, kampuni tatu ziliruma maombi ambapo moja kutoka Afrika Kusini ya M/S Ren-Form CC iliibuka mshindi.
Soma zaidi:-
Ufafanuzi huo wa Dk. Mahera unatokana na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuwa, NEC imefanya mabadiliko ya mchapishaji kinyume na taratibu.
Mnyika alisema, NEC imeiteua kinyemela Kampuni ya Jamama akidai mmoja wa wamiliki wake ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Soma taarifa yote ya Dk. Mahera hapa chini;
Leave a comment