Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC watangaza uchaguzi jimbo la Waitara
Habari za SiasaTangulizi

NEC watangaza uchaguzi jimbo la Waitara

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo tarehe 4 Agosti, 2018 imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika majimbo matatu na wa udiwani katika kata mbili za Tanzania Bara utakaofanyika Septemba 16, mwaka huu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Akitangaza uchaguzi huo mjini Dodoma leo, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mbarouk Salim Mbarouk amesema fomu za uteuzi wa wagombea wa Majimbo hayo zitatolewa kuanzia tarehe 13 hadi 20 Agosti, 2018 na uteuzi utafanyika tarehe 20 Agosti, mwaka huu wakati kampeni zitaanza tarehe 21 Agosti na kumalizika tarehe 15 Septemba, mwaka huu.

“Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo matatu,” amesema Jaji Mbarouk.

Jaji Mbarouk ameyataja majimbo hayo kuwa ni Korogwe Vijijini, Mkoa wa Tanga kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ndugu Stephen Hilary Ngonyani, Jimbo la Ukonga Katika Mkoa wa Dar Es Salaam na Jimbo la Monduli katika Mkoa wa Arusha

Amesema wabunge wa majimbo hayo mawili Ndugu Mwita Mwikabe Waitara na Ndugu Julius Kalanga Laizer wajiuzulu uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hivyo kupoteza sifa za kuwa Wabunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Regina Mkonde: CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

error: Content is protected !!