Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC: Tutaanza kuchukua hatua kali kwa…
Habari za Siasa

NEC: Tutaanza kuchukua hatua kali kwa…

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imewataka wagombea ubunge na udiwani waliokata rufaa kuwa na subra  wakati rufaa hizo zikishughulikiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Pia, NEC imetoa onyo kwa wanasiasa wanaotoa lugha zisizositahili kwenye majukwaa ya kampeni kuwa wataanza kuchukua hatua kali ikiwemo kusitisha mikutano yao ya kampeni. 

Hayo yamesemwa leo Jumanne tarehe 15 Septemba 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera wakati akifungua mkutano wa tume hiyo na watao huduma ya habari mtandaoni unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Dk. Mahera amesema, uchaguzi ni mchakato unaohusisha mambo mengi ikiwemo uteuzi wa wagombea, uandikishaji wapiga kura na kampeni za uchaguzi.

Amesema, baada ya uteuzi wa wagombea, walipokea rufaa zaidi ya 500 za wagombea ubunge na udiwani ambazo wanaendelea kuzifanyia kazi na wanatarajia kuzimaliza kesho Jumatano.

“Wanapokuwa wanatoa matamko yao kuwa tunachelewa kutoa uamuzi wa rufaa watambue tunazifanyia kazi kwa kuzichambua kwa kina ili tuweze kutenda haki.”

“Tungepokea rufaa na kukubaliana nazo tungekuwa tumemaliza kuzitolea uamuzi, kwa hiyo watambue tunaendelea kuzifanyia kazi kwa umakini mkubwa na kesho tutamaliza,” amesema Dk. Mahera

Kauli ya Dk. Mahera ameitoa ikiwa ni siku moja imepita tangu John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema aliitaka Tume hiyo kutoa rufaa hizo haraka ili wahusika waanze kampeni.

Jana Jumatatu, Mnyika alisema, rufaa zao wameziwasilisha NEC lakini hakuna majibu yanayotoka jambo linaloweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Katika mkutano huo, Dk. Mahera amesema, kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa kutumia lugha zisizotakiwa kwenye kampeni ambazo zinakwenda kinyume na maadili hali ambayo hawatokubali kuona zinaendelea.

Amesema, wanasiasa wanapaswa kutumia kipindi hiki kunadi sera na ilani zao kwa wananchi ili waweze kuwachagua na si kutukana, kuchochea vurugu au kukejeli wagombea wengine.

“Kuanzia sasa hivi, tutachukua hatua kali kwa wanaotoa lugha kali ikiwemo kumfungia kupiga kampeni na hata ukipiga kelee kwa mjomba huko nje hatutakusikia. Kwa hiyo, wanasiasa wanapaswa kutumia lugha zenye staha,” amesema Dk. Mahera

Pia, ametumia fursa hiyo kuvitaka vyombo vya habari kuhakikisha vinatoa elimu kwa umma kuhusu uchaguzi huo huku kuzingatia kulinda amani ya nchi kabla na baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!