Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera

NEC: Kura ya Rais itapigwa ulipojiandikisha

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), amewataka wananchi kubaki maeneo waliyojiandikisha kupiga kura, ili wapate nafasi ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yamesemwa na Dk. Wilson Mahera,Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu upigaji kura kwa wagombea wa nafasi za Urais wa Tanzania.

“Tunawasihi wale waliojiandikishia kwenye vituo vyao kubaki masneo hayo sababu sheria ya uchaguzi inaeleza mtu anapiga kura katika kituo alichojiandikishia.”

“Tunawasihi wajitahidi kadri watakavyoweza kuwa kwenye maeneo waliyojiandikishia ili wapate nafasi ya kupiga kura ya urais,” amesema Dk. Mahera.

Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura

Dk. Mahera amesema, taarifa ya kwamba mpiga kura anaweza kupiga kura za kuchagua mgombea wa urais kwenye kituo ambacho hakujiandikisha, si za kweli na kwamba Sheria ya Uchaguzi inaelekeza watu wapige kura katika vituo vyao husika.

“Kumekuwepo na changamoto watu wamekuwa wakiuliza maswali kupiga kura ya urais unapiga kura mahali popote, Kama mtu amejiandikisha kwa mfano kupiga kura mara akapiga Dodoma si kweli,” amesema Dk. Mahera.

Hata hivyo, Dk. Mahera amesema, wanaoruhusiwa kupiga kura katika vituo ambavyo hawajajiandikishia ni watendaji wa NEC ambao wanapewa barua za kibali na wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo husika.

“Fursa kwa wale watendaji walioajiriwa na tume kwa madhumuni ya uchaguzi huu na wanakuwa na mkataba, lakini na wao inakuwa na mipaka yake na wao ni yule amejiandikisha kwenye jimbo husika au wilaya husika,” amesema Dk. Mahera na kuongeza:

“Kama wilaya ina majimbo mawili basi kwenye wilaya husika na alijiandikisha jimbo A wakati anafanya kazi jimbo la B ataweza piga kupata kibali cha kupiga kura ya urais.”

TUME ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), amewataka wananchi kubaki maeneo waliyojiandikisha kupiga kura, ili wapate nafasi ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). Hayo yamesemwa na Dk. Wilson Mahera,Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu upigaji kura kwa wagombea wa nafasi za Urais wa Tanzania. “Tunawasihi wale waliojiandikishia kwenye vituo vyao kubaki masneo hayo sababu sheria ya uchaguzi inaeleza mtu anapiga kura katika kituo alichojiandikishia." "Tunawasihi wajitahidi kadri watakavyoweza kuwa kwenye maeneo waliyojiandikishia ili wapate nafasi ya kupiga kura ya urais,” amesema Dk. Mahera. Wananchi wakiwa katika…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!