RAIS John Magufuli amemteua Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Damas Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Dk. Susan Kolimba. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).
Dk. Ndumbalo anachukua nafasi ya Dk. Susan ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa leo tarehe 26 Septemba 2018 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Vile vile, taarifa hiyo inaeleza kuwa, Rais Magufuli amemteua Dkt. Faraji Mnyepe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Prof. Mkenda amechukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi ambaye amestaafu.
“Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 26 Septemba, 2018 na tarehe ya kuapishwa kwao itatangazwa baadaye,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Leave a comment