Akram Aziz, akitoka mahakamani Kisutu

Ndugu wa Rostam Aziz afutiwa mashitaka

NDUGU wa mfanyabiashara mashuhuri nchini, Rostam Aziz, anayefahamika kwa jina la Akram Aziz, amefutiwa mashitaka na serikali. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akram alifunguliwa mashitaka mahakamani tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Alituhumiwa kukutwa na nyara za serikali, ujangili, utakatishaji wa fedha, udangaanyifu na kujimilikisha silaha kinyume cha sheria.

Mbele ya Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu, upande wa mashitaka uliwasisha hoja ya kumfutia mtuhumiwa huyo mashitaka yote yaliyokuwa yanamkabili.

Hata hivyo, alizuiwa kuondoka mahakamani hapo. Inadaiwa kuwa serikali imepanga kubadilisha hati yake ya mashitaka ili kuweza kumfungulia mashitaka mengine.

NDUGU wa mfanyabiashara mashuhuri nchini, Rostam Aziz, anayefahamika kwa jina la Akram Aziz, amefutiwa mashitaka na serikali. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). Akram alifunguliwa mashitaka mahakamani tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Alituhumiwa kukutwa na nyara za serikali, ujangili, utakatishaji wa fedha, udangaanyifu na kujimilikisha silaha kinyume cha sheria. Mbele ya Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu, upande wa mashitaka uliwasisha hoja ya kumfutia mtuhumiwa huyo mashitaka yote yaliyokuwa yanamkabili. Hata hivyo, alizuiwa kuondoka mahakamani hapo. Inadaiwa kuwa serikali imepanga kubadilisha hati yake ya mashitaka ili kuweza kumfungulia mashitaka mengine.

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram