Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai

Ndugai amwaga sumu kampeni za CCM

Spread the love

JOB Ndugai, mbunge mteule wa Jimbo la Kongwa, Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewataka Watanzania kuwapuuza wagombea wa vyama vya upinzani nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea.

Amesema, endapo Watanzania watawachagua wagombea hao, watakuwa wanamilikiwa na viongozi wa vyama vyao badala ya kutumikia wananchi.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni za Urais za CCM leo tarehe 29 Agosti 2020 jijini Dodoma, Spika Ndugai amesema, wabunge kupitia upinzani kazi yao ni kususa bungeni.

“Kwa hiyo lazima wbaunge wetu wa CCM wawe wengi na wale wengine lazima niwape ripoti kazi yao ni kususa, kununa na  kutoka nje bungeni.

“Sidhani kama Watanzania mnachagua watu kwenda bungeni au kutoka bungeni, badala kuwa mali yenu wananchi, wanakuwa mali ya vyama, hilo tuliangalie sana,” amesema Spika Ndugai.

John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM

Wakati huo huo, Spika Ndugai amemueleza Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli kwamba maandalizi ya Bunge la 12 yanakaribia ukingoni, na kwamba litakuwa la kisasa kuliko la 11.

“Mwenyekiti mimi ndio muandaaji wa Bunge la 12 , nikwambie mapema kwamba maandalizi yetu ya Bunge la 12 ambayo litakuwa la kisasa zaidi ya 11 yako kwa zaidi ya asilimia 80,” amesema Spika Ndugai.

JOB Ndugai, mbunge mteule wa Jimbo la Kongwa, Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewataka Watanzania kuwapuuza wagombea wa vyama vya upinzani nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea. Amesema, endapo Watanzania watawachagua wagombea hao, watakuwa wanamilikiwa na viongozi wa vyama vyao badala ya kutumikia wananchi. Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni za Urais za CCM leo tarehe 29 Agosti 2020 jijini Dodoma, Spika Ndugai amesema, wabunge kupitia upinzani kazi yao ni kususa bungeni. “Kwa hiyo lazima wbaunge wetu wa CCM wawe wengi na wale wengine lazima niwape ripoti kazi yao ni kususa, kununa na  kutoka nje bungeni. “Sidhani kama Watanzania mnachagua watu kwenda…

Review Overview

User Rating: 4.3 ( 1 votes)

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!