Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai amtaka Profesa Assad ajiuzulu
Habari za Siasa

Ndugai amtaka Profesa Assad ajiuzulu

Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spread the love

JOB Ndugai Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  ameshauri  Professa Mussa Assad Mkaguzi na Mdhibiti  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ajiuzulu. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Ndugai amesema kuwa Profesa Assad amelinajisi bunge na kwamba bunge halina imani naye hivyo ajiuuzulu ili asimpe wakati mgumu Rais John Magufuli.

“Azimio la bunge ni halali …katika nchi za wenzetu bunge likikuwa halina imani na wewe hung’ang’ani unajiuzulu sisi hatumfundishi lakini anampa wakati mgumu Rais . ..aende kwa Rais amueleze rais kwamba aliteleza ..matusi hayo anayoyatoa kwa Bunge anamtukana kila mtu, Rais yupo mule, mawaziri wapo mule anautukana hadi mkono unaomlisha .. anauthubutu jasiri na ni shujaa lakini ushajaa wake ni wa Mbwa kung’ata anayempa chakula.”

Amesema kuwa bunge halijachukuziwa  na Ripoti ya (CAG) kutokana na bunge halijaguswa na ripoti hiyo  tatizo ni maneno aliyoyatumia CAG kuliita Bunge Dhaifu.

“Neno dhaifu kihasibu mkaguzi analitumia kwa taasisi anayoikagua na kuwatumia washika dau anaofanyia kazi na washika dawa hapa ni bunge kwa ajili ya wananchi anachosema serikali  anaelekeza anapoelekeza anaogopa kusema yeye amewekwa na serikali kwa ajili ya kuangalia na kutuambia sisi hawezi tena kugeuka na kufanya alichofanya” amesema.

Amesema kuwa Profesa Assad ameendelea na msimamo wake wa kuliita Bunge Dhaifa pale alipohojiwa na Kamati ya Bunge na hata alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa jina hilo Bunge halipendezwi nalo lakini bado Profesa Assad analitumia “Hata katika maisha ya kawaida  mtu anakuambia jina fulani silipendi anaendelea kukuita. Akaambiwa toa kamusi yako ya kiswahili neno lile ni neno lisilokuwa na heshima kwa bunge.

“Neno ambalo hatulipendi unalipenda jiite wewe na kuonyesha kuwa hatulipendi tukalichukulia hatua hata wenzetu . Kurudia na kuahidi utarudia tutakuita tena.” Amesema Ndugai.

Wakati huo huo  Ndugai ametoa ufafanuzi juu ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bunge  wiki  iliyopita  kuwa ni Maswali juu ripoti ile kwa maana Kamati za Bunge zitatoa ripori kamili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!