NDEGE ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 149 na wafanyakazi wa ndege nane, ilipata ajali hiyo kuda mchache baada ya kuruka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Adis Ababa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo la ndege inasema kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya Bishoftu nje kidogo ya jiji la Adis Ababa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa ndege hiyo yenye usajili ET-AVJ iliruka uwanjani hapo leo saa 2:36 lakini ilipoteza mawasiliano saa 2:44 na baadavya muda kugundulika imepata ajali.
Pia taarifa hiyo haijathibitisha ni watu wangapi wamefariki kufuatia ajali hiyo na imewataka ndugu wa abiria waliosafiri na ndege hiyo wawe watulivu mpaka hapo watakapotoa taarifa rasmi.
Ofisi ya waziri Mkuu wa Ethiopia, Abey Ahmed imethibitisha kutokea kwa ajali hiuo na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za walio wapoteza wapendwa wao katika jali hiyo.
The Office of the PM, on behalf of the Government and people of Ethiopia, would like to express it’s deepest condolences to the families of those that have lost their loved ones on Ethiopian Airlines Boeing 737 on regular scheduled flight to Nairobi, Kenya this morning.
— Office of the Prime Minister – Ethiopia (@PMEthiopia) March 10, 2019
Leave a comment