June 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nchi Jumuiya Afrika Mashariki zakubaliana kupunguza tozo

Ukur Yatani, Waziri wa Fedha wa Kenya

Spread the love

NCHI zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zimependekeza viwango vipya na kuondoa tozo za ushuru wa pamoja wa forodha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Hayo yameainishwa leo tarehe 11 Juni 2020 na Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.

Dk. Mpango amesema, mapendekezo hayo kutoka asilimia 25 hadi 0, yametokana na kikao cha Mawaziri wa Fedha wa jumuiya hiyo tarehe 13 Mei 2020 kwa njia ya mtandao.

“Mapendekezo ya Mawaziri wa Fedha ya kufanya marekebisho kwenye Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa Forodha yanahusisha hatua mpya na zinazoendelea ambazo zimekuwa zikitekelezwa katika mwaka 2019/20,” amesema Dk. Mpango.

Jumuiya hiyo imekubaliana kuondoa tozo za ushuru wa malighafi zinazotumika kutengeneza vifaa maalum vya kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19), zilizokuwa zikitozwa asilimia 25 hadi 10.

Ametaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na barakoa, kipukusi (Sanitizer)mashine za kusaidia kupumua, mavazi ya kitabibu (PPE).

Matia Kasaija, Waziri wa Fedha Uganda

Amesema, nchi hizo zimekubaliana kuondoa  ushuru wa mashine za kielektroni za ukusanyaji kodi (EFD), kutoka asilimia 10.

Pia kuondoa asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vinavyotumiwa na wazalishaji wa maziwa kwa joto la juu yanayodumu kwa muda mrefu (UHT Milk).

“Tozo ya vifuniko vya chupa za mvinyo vimependekezwa kuondolewa kutoka asilimia 10, kwa lengo la kupunguza gharama ya uzalishaji wa zao la zabibu.

“Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia kahawa vinavyotumiwa na viwanda vya kusaga kahawa nchini,” amesema Dk. Mpango.

Amesema, kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia korosho.

Mawaziri hao pia wamekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia pamba.

Wakati huo huo jumuiya hiyo imependekeza ongezeko la ushuru wa forodha kwenye maeneo yafuatayo;-

Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za marumaru zinazoingizwa kutoka nje kwa  Lengo la kukuza viwanda vya ndani vinavyozalisha marumaru.

Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye chai inayotoka nje.

Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na MIpango Tanzania

“Lengo la pendekezo hili ni kulinda viwanda vya ndani na kuhamasisha kilimo cha chai hapa nchini pamoja na kuongeza ajira katika sekta ya kilimo”,ameeleza Dk Mpango.

Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye magunia yanayotoka nje kwa lengo la kukuza viwanda vya ndani.

Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 0 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye kakao inayoingizwa kutoka nje.

“Lengo ni kuchochea na kuhamasisha kilimo cha zao la kakao nchini pamoja na kuongeza mapato ya Serikali”, amesema Dk Mpango.

error: Content is protected !!