NCCR-Mageuzi yamteua Maganja kugombea urais, Z’bar wakosa

Spread the love

YEREMIA Kurwa Maganja ameteuliwa na Mkutano Mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha NCCR-Mageuzi kugombea urais wa nchi hiyo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkutano huo umefanyika leo Ijumaa tarehe 7 Agosti 2020 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kuongozwa na James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi, Anthony Komu amesema, wajumbe waliopiga kura walikuwa 258. Kura saba zimeharibika, kura 20 zimepugwa hapana “na kura 231 zimepigwa ndiyo sawa na asilimia 89. Kwa hiyo namtangaza Yeremia Kurwa Maganja kuwa mgombea wetu urais.”

Baada ya kutangaza matokeo hayo, Maganja aliyejiunga na NCCR-Mageuzi akitokea ACT-Wazalendo alikokuwa mwenyekiti wa chama hicho, amepewa fursa kwa mujibu wa katiba yao kumtangaza mgombea wake mwenza, Haji Ambari Khamisi.

Itakumbukwa, Khamisi alikuwa amechukua fomu ya kuwania urais wa Zanzibar lakini ndani ya mkutano huo atangaza kujitoa akisema umri umekwenda.

Awali, Komu alisema kutokana na Zanzibar kutokuwa na mgombea, Maganja ataona vyama ambavyo watashirikiana katika nafasi ya urais.

YEREMIA Kurwa Maganja ameteuliwa na Mkutano Mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha NCCR-Mageuzi kugombea urais wa nchi hiyo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Mkutano huo umefanyika leo Ijumaa tarehe 7 Agosti 2020 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kuongozwa na James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi. Akitangaza matokeo ya uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi, Anthony Komu amesema, wajumbe waliopiga kura walikuwa 258. Kura saba zimeharibika, kura 20 zimepugwa hapana “na kura 231 zimepigwa ndiyo sawa na asilimia 89. Kwa hiyo namtangaza Yeremia Kurwa Maganja…

Review Overview

User Rating: 3.35 ( 1 votes)

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!