Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nasikia naitwa polisi, ngoja niende – Lema
Habari za Siasa

Nasikia naitwa polisi, ngoja niende – Lema

Spread the love

GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, leo tarehe 14 Novemba 2019 amesema, amepewa taarifa za wito wa Jeshi la Polisi wilayani Hai, Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Polisi wamevamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Halmshauri Hai, Helga Mchomvu, wamemkamata dereva wangu na gari yangu nyumbani kwa Helga, Nimepewa taarifa kuwa, ninatafutwa. Nimeamua kuelekea Kituo cha Polisi Hai,” Lema ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, wito wa Lema kwenda polisi umetolewa na Lengai Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai akidai kwenda kufanya njama za vurugu kwenye wilaya yake.

Taarifa zinaeleza, Lema alikuwa Hai kufanya vikao vya ndani vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na kwamba vitendo vya wanasiasa kutoka maeneo yao na kwenda maeneo mengine vimezuiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!