Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nani kupenya kugombea urais, ubunge Tanzania?
Habari za SiasaTangulizi

Nani kupenya kugombea urais, ubunge Tanzania?

Spread the love

MACHO na masikio ya Watanzania wengine yanaelekezwa Jiji la Dodoma kutakakofanyika uteuzi wa wagombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Uteuzi huo unafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika ofisi zake zilizopo Ndejembi nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Pia, kesho hiyohiyo kutafanyika uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani nchini nzima.

Uteuzi wa urais, hii ni mara ya kwanza, NEC kuendesha shughuli hiyo Dodoma baada ya kuhamia huko ikitokea jijini Dar es Salaam.

Joto la wagombea 17 waliochukua fomu zinapanda na kushuka wakisubiri kuona Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itamteua nani na kumwacha nani.

Idadi hiyo ya wagombea ni kubwa kulizo zilizowahi kujitokeza kwenye chaguzi tano zilizopita ambapo uchaguzi mkuu wa mwisho mwaka 2015 walijitokeza wagombea 11.

Bernard Membe-ACT-Wazalendo

Hata hivyo, NEC iliwateua wagombea nane waliokidhi vigezo, wawili hawakurejesha fomu huku mmoja akirejesha nje ya muda uliokuwa umepangwa.

Kati ya hao nane walioteuliwa, mwanamke alikuwa mmoja ambaye ni Anna Mgwhira aliyegombea kupitia chama cha ACT- Wazalendo.

Anna ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, tarehe 3 Juni 2017, Rais Magufuli alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro nafasi anayohudumu mpaka sasa.

Mwaka huu, ni vyama viwili pekee vyenye usajili wa kudumu vya TLP na UDP havijajitosa kwani vilitangaza kumuunga  mkono mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Magufuli.

Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji fomu ulianza tarehe 5 Agosti na utahitimishwa kesho Jumanne.

Kampeni za uchaguzi huo zitaanza tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020 ikiwa ni siku 62.

Kati ya wagombea 17 waliochukua fomu, wanawake ni wawili ambao ni Cecilia Augustino Mwanga wa chama cha Demokrasia Makini na Qeen Cuthbert Sendiga wa chama cha ADC  huku wagombea wenza kati ya 17 ni watano.

Wengine ambao wanasubiri kuona kama wateteuliwa na NEC ni; Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi), Seif Maalim Seif (AAFP), Leopard Mahona (NRA), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Philip John Fumbo (DP) na David Mwaijojele wa Chama Cha Kijamii (CCK).

Pia wamo; Khalfan Mohamed Mazurui (UMD), Twalib Ibrahim Kadege (UPDP), Rais John Pombe Magufuli (CCM), Bernard Membe (ACT- Wazalendo), Tundu Lissu (Chadema), Mutamwega Bati Mgaiwa (SAU), Hashim Rungwe (Chaumma) na John Shibuda wa Ada Tadea.

Qeen Cuthbert Sendiga-ADC

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu, Semistocles Kaijage amesema amezungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma akisema, tume hiyo itafanya uteuzi kesho Jumanne kwa wagombea urais, wabunge na madiwani nchi nzima.

Amesema, uteuzi wa wagombea urais na makamu utafanyikia ofisi za NEC zilizopo Njedengwa jijini Dodoma.

“Uteuzi wagombea urais na makamu utafanyikia kesho ofisi za tume zilizopo Dodoma. Ubunge utafanyika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo husika na kwa udiwani utafanyika ofisi za wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata.”

Cecilia Augustino Mwanga wa Demokrasia Makini

“Baada ya uteuzi, fomu zitabandikwa katika mbao za matangazo za ofisi iliyohusika na uteuzi,” amesema

Jaji Kaijage amesema “Tume inaelekeza na inasisitiza wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kuwepo ofisi zao kesho wakati wote kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 10 jioni.”

Mwenyekiti huyo amesema “kitendo cha kutokuwepo ofisini katika muda huo, kitapelekea tume kuchukua hatua kali dhidi ya watendaji wa majimbo na kata husikika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!