Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Naibu Spika ajitosa Urais Z’bar, wagombea wafikia 31
Habari za SiasaTangulizi

Naibu Spika ajitosa Urais Z’bar, wagombea wafikia 31

Spread the love

MGENI Hasaan Juma, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, amechukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)

Mgeni amekuwa mwanamke wa nne kujitosa katika kinyang’anyiro hicho ambacho wagombea wamefika 31 ambao wamejitosa kutaka kumrithi Rais Ali Mohamed Shein.

Katika uchaguzi huo wa Oktoba 2020, Rais Shein hatogombea kwani amemaliza muhula wake wa miaka kumi kwa mujibu wa Katiba.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu Ofisa Kuu ya CCM Zanzibar, Mgeni alikwenda kuomba dua katika kaburi la Hayati Abeid Aman Karum, Rais wa kwanza wa Zanzibar kisha kupata fursa ya kuongea na waandishi wa habari.

Mwantum Mussa Sultan akiwa na fomu za kuwania Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Amesema, amejitokeza katika mbio hizo ili kuwatia moyo wanawake wengine kutokana na yeye mwenyewe kuwa ni miongoni mwa wanawake viongozi na wanaharakati wa wanawake.

Mgeni amesema, kitendo cha kujitokeza wagombea 30 kinaonyesha jinsi ndani ya chama hicho kuna demokrasia.

Naibu spika huyo amesema, ujio huo ni kutekeleza kauli mbio ya 50 kwa 50.

Hasna Atai Masoud

Aidha, almesema, amekuwa katika nafasi mbalimbali ikiwemo sekta binafsi, mwalimu na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Wanawake wengine waliojitosa katika mbio hizo ni; Fatma Kombo Hassan, Hasna Attai Masoud na Mwatum Mussa Sultan.

Uchukuaji na urejeshaji fomu hizo ulianza tarehe 15 hadi 30 Juni 2020 ambapo tayari zaidi ya wagombea 15 wamerejesha fomu.

Fatma Kombo Masound

Wagombea wote 31 waliojitokeza ni;

1. Mbwana Bakari Juma
2. Balozi Ali Abeid Karume
3. Mbwana Yahya Mwinyi :
4. Omar Sheha Mussa
5. Dk. Hussein Ali Mwinyi
6. Shamsi Vuai Nahodha
7. Mohammed Jaffar Jumanne
8. Mohammed Hijja Mohammed
9. Issa Suleiman Nassor
10. Profesa Makame Mnyaa Mabarawa
11. Mwatum Mussa Sultan
12. Haji Rashid Pandu
13. Abdulhalim Mohammed Ali
14. Jecha Salum Jecha
15. Dk. Khalid Salum Mohammed
16. Rashid Ali Juma
17. Khamis Mussa Omar
18. Mmanga Mjengo Mjawiri
19. Hamad Yussuf Masauni
20. Mohammed Aboud Mohammed
21. Bakari Rashid Bakari
22. Hussein Ibrahim Makungu
23. Ayoub Mohammed Mahmoud
24. Hashim Salum Hashim
25. Hasna Atai Masound
26. Fatma Kombo Masound
27. Iddi Hamadi Iddi
28. Pereira Ame Silima
29. Shaame Simai Mcha
30. Mussa Aboud Jumbe
31. Mgeni Hasaan Juma

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!